kikosi cha timu ya mchezo wa mpira wa pete ya Taswa Dar mara baada ya mechi kuisha.
Siku
moja kabla ya bonanza waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha walipata
fursa ya kutembelea kiwanda cha bia ya TBL Arusha hapa mmoja wa
wafanyakazi wa kampuni hiyo akiwa anawapa maelekezo ya jinsi kiwanda
hicho kinavyoweza kufanya kazi ya kutengeneza beer kwa kutumia mashine
na komputa
nikiwa
na waandishi wa habari wakogwe mara baada tu ya kuwasili ndani ya
kiwanda cha bia cha Tbl Arushawa kwanza kushoto ni Gwandu akifuatiwa na
Woinde shizza,Mr mchau wakwanza kulia ni Salma Mchovu pamoja na
Yasinta..
waandishi wahabari wa mkoa wa Arusha wakifurahia wakati tamasha likiendelea
Na Woinde shizza,Arusha
TIMU
ya soka ya chuo cha uandishi wa habari Arusha(AJTC) juzi walitwaa
ubingwa katika bonanza la 10 vyombo vya habari mkoani Arusha huku Timu
ya wanahabahari wa Dar es Salaam TASWA FC wakishindwa kutamba.
Katika Bonanza hilo, ambalo lilishirikisha jumla ya timu nane, TASWA FC) alishindwa kutamba na kushika nafasi ya nne, Hata hivyo timu ya wanahabari wasichana kutoka Dar es Salaam(TASWA Qeen) iliweza kutwaa ubingwa wa mpira wa pete.
Katika Bonanza hilo, ambalo lilishirikisha jumla ya timu nane, TASWA FC) alishindwa kutamba na kushika nafasi ya nne, Hata hivyo timu ya wanahabari wasichana kutoka Dar es Salaam(TASWA Qeen) iliweza kutwaa ubingwa wa mpira wa pete.
Katika bonanza hilo, lililofanyika Uwanja wa Sheikh
Amri Abeid mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda
,AJTC walitwaa ubingwa baada ya kujikusanyia alama saba huku nafasi ya
pili, ikichukuliwa na timu ya wanahabari kutoka mkoa wa Manyara wa kituo
cha radio ORS.
Chuo
cha habari cha IMS kilishika nafasi ya tatu ,kikifuatiwa na TASWA Dar,
TASWA Arusha, MJ Radio,Arusha One radio na radio Habari Maalum.
Mkuu
wa mkoa wa Arusha, Filex Ntibenda aliwakabidhi mabingwa wa soka kikombe
na fedha taslim Tsh 250,000, huku washindi wa pili wakipata fedha
taslimu 150,000 na kikombe.
Katika
Tamasha hilo, timu ya TASWA Qeen ilikabidhiwa kikombe na Tsh 150,000,
huku timu ya pili AJTC Qeen ikipata fedha taslim 10000 na kikombe.
TASWA FC ilipata zawadi ya timu yenye nidhamu katika michuano hiyo na kupokea zawadi na fedha taslimu 50,000.
Akizungumza wakati akifunga bonanza hilo, Ntibenda alipongeza TASWA Arusha na kampuni ya Arusha media kwa kuandaa Bonanza hilo.
Aliwataka wanahabari kuwa na tabia ya kushiriki katika michezo kwani michezo hujenga, Afya na ni ajira.
Mkuu
wa mkoa wa Arusha, pia alikabidhi vyeti vya udhani Bonanza hilo ,
kampuni ya bia nchini(TBL), Shirika la hifadhi ya Taifa TANAPA, kampuni
ya Mega Trade.
Shirika la nyumba la Taifa(NHC),Kampuni ya Tanzanite One, Big Expedition, Taasisi ya Faidika, Kampuni ya Pepsi na Coca cola.
No comments:
Post a Comment