Watanzania
wametakiwa kutafakari kwa kina kauli iliyotolewa na mgombea wa kiti cha
urais kupitia UKAWA Mh Edward Lowassa ya kuwaachia huru baadhi ya
watuhumiwa wa makosa ya kigaidi yaliyosababisha vifo na ulemavu wa
kudumu kwa baadhi ya viongozi wa dini wa kiislamu na kikristo pamoja na
wageni kutoka nje ya nchi sambamba na watuhumiwa wengine wa makosa ya
kijinai bila kujali athari zinazosababishwa na matukio ya kigaidi
ulimwenguni.
Tahadhari
hiyo imetolewa mjini Ludewa mkoani Njombe Bwana Amoni Mpanju wakati
akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kusikiliza sera za Dr
Magufuli na kuongeza kuwa wakati dunia ikihaha kupambana na janga la
matukio ya kigaidi yanayosababisha vifo na ulemavu wa kudumu kwa
binadamu bila ya kujali imani zao za kidini na mataifa yao baadhi ya
viongozi wanaowania kuliongoza taifa la Tanzania wanatangaza hadharani
kuwaachia huru watuhumiwa wa ugaidi waliosababisha vifo na majeruhi kwa
viongozi wa dini za kikristo na kiislamu na wageni wa mataifa mengine na
kuwataka watanzania kutafakari kauli hiyo ya Mh Lowassa.
Dr
John Pombe Magufuli akiwa katika ubora wake amefanya mikutano zaidi ya
mitano akiwa njiani kutoka mkoano Njombe kuelekea Ludewa Songea kwa njia
ya barabara ambapo amekuwa pia akisikiliza kero za walemavu alioonana
nao na kuongeza kuwa uongozi ni msalaba na si kila mtu anaweza
kuwatumikia kwa dhati wananchi na kwamba kiongozi anapaswa kuzifahamu
kero za wananchi na kuziishi na kwamba ili Tanzania iwe na amani ni
lazima majeshi yetu yaendeshwe kisayansi na kuahidi kuayaboresha.
Aidha
Dr Magufuli ambaye amekuwa akishangiliwa na umati mkubwa wa wananchi
waliokuwa wanaziba barabara kwa lengo la kutaka kumsikia amewataka
wananchi kumchagua yeye kupitia CCM kwa kuwa ndio chama chenye ilani
bora na ahadi za ukweli huku akiwazodoa UKAWA kwa kutokuwa na ilani
ambayo ni mkataba kati ya watawala na watawaliwa.
Dr
Magufuli anatarajiwa kuendelea na ziara yake ya kusaka ridhaa ya
watanzania kuliongoza taifa la Tanzania ambapo jumatatu ya Septemba mosi
anatarajiwa kuendelea na kampeni zake mkoani Ruvuma
No comments:
Post a Comment