…………………………………..
Wanawake Wachimbaji wa madini kutoka mikoa ya Tanga,Singida
,Manyara na Morogoro wameiomba serikali ipunguze ada ya leseni ya
uchimbaji madini ili kuwawezesha kinamama wanaoanza kazi hiyo
wasikwame kiuchumi kutokana na kukabiliwa na changamoto ya bei kubwa ya
vifaa vya uchimbaji pamoja na ukosefu wa mitaji.
Kinamama hao ambao wameamua kujikita kwenye shughuli za
uchimbaji wa madini wameiomba serikali isikie kilio chao cha muda mrefu
licha ya sekta hiyo ngumu bado inawasaidia kinamama kujikwamua kiuchumi
na kuondokana na umasikini.
Pili Hussein ni mwanamama wa kwanza kuzama katika migodi ya
Mirerani na kuchimba madini ambaye kwa sasa ni mmiliki wa kitalu cha
madini amesema kuwa gharama kubwa za uendeshaji wa migodi zimekua
zikirudisha nyuma juhudi za kinamama hivyo ameiomba serikali na
mashirika binafsi kujitokeza kuwasaidia kinamama kupata mikopo
itakayoiwasaidia kuendesha shughuli za uchimbaji
Wakizungumza katika jukwaa la kinamama wachimbaji wa madini
linaloendelea mkoani Kilimanjaro lilioandaliwa na shirika lisilokuwa
la kiserikali la Hakimadini ,jukwaa lenye lengo la kuunganisha sauti na
nguvu ya kinamama katika kutetea haki zao hususan katika sekta ya
madini na kunufaika ipasavyo,Mwansy Shomari ni Mchimbaji wa Madini aina
ya Ruby kutoka eneo la Kalalani mkoani Tanga amesema kuwa licha ya
changamoto wanazozipitia mfumo dume umekua ukiwakwamisha kinamama kupiga
hatua kiuchumi hususani katika sekta ya madini iliyotawaliwa na mfumo
dume kwa kipindi kirefu
Kwa upande wake Meneja Programu wa Shirika la Hakimadini
,David Ntiruka amesema kuwa wameanzisha program maalumu ya kukusanya
sauti ya kinamama wachimbaji pamoja na changamoto zao ili kuzifikisha
kwenye vyombo husika viweze kufanyiwa kazi
Mwamko wa wanawake kujihusisha na shughuli za uchimbaji
madini bado unakua na kuongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo
wanawake wachache walithubutu kujihusisha na uchimbaji ,kutokana na
kuongezeka kwa uelewa juu ya haki ya kunufaika na madini kwa jinsia zote
wanawake wengi wanashiriki katika uchimbaji madini.
No comments:
Post a Comment