Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, February 26, 2015

MKUU WA MKOA WA NJOMBE AFUNGUA MAFUNZO YA SIKU SITA KWA WAKUU WA SHULE WA MIKOA YA MBEYA NA NJOMBE

 
 MKUU WA MKOA WA NJOMBE AKIWA KATIKA UKUMBI WA TURBO AKITOA HOTUBA YAKE  KWA WAKUU WA SHULE


 MAAFISA ELIMU WA SHULE YA SEKONDARI KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE  VENANCE MSUNGU  WA PILI KUTOKA KULIA NA  MSINGI  Zegeli Shengelo WAKIWA NA MUWAKILISHI TOKA ADEMU

 MRATIBU WA MAFUNZO TOKA ADEMU ESTER  JONAS AKISOMA RISALA FUPI KWA MGENI RASMI


 RC NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI AKIZUNGUMZA




Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Ameziagiza Halmashauri Zote Za Mkoa Wa Njombe  Kutenga Maeneo Ya Viwanja Kwaajili Ya Watumishi Wa Elimu  Hususani Walimu Ikiwa Ni Pamoja Na Kuwajengea Nyumba Ili Watakapo Staafu Waweze Kuwa Na Sehemu Za Kuishi.

Dkt Nchimbio Ametoa Agizo Hilo Wakati Wa Ufunguzi Wa Semina Ya Siku Sita Kwa Wakuu Wa Shule Za Sekondari Za Serikali Na  Za Watu Binafsi  Kinachofanyikia Katika Ukumbi Wa Turbo  Tangu Februari 23  Ambapo Semina Hiyo Imeandaliwa Na Watu Wa Ademu

Aidha Dkt Nchimbi Amesema Kuwa Ofisi Ya Mkoa Wa Njombe  Inatarajia Kuandaa Tuzo Kwa  Viongozi Wakuu  Katika Sekta Ya Elimu  Ambapo Amesema Hali Hiyo Itasaidia Kuwapa Motisha Na Moyo Wa Kufundisha  Na Kuondoa Manung'uniko  Miongoni Mwa Baadhi Ya  Wakuu Hao.

Katika Hatua Nyingine Dkt Nchimbi  Amewataka Wamiliki Wa Shule Za Watu Binafsi Kuwa Shirikisha Viongozi Wa Serikali Katika Kushirikiana Kutatua Baadhi Ya Changamoto Zinazowakabili  Huku Wakitakiwa Kuweka Mazingira Rafiki Kwa Watumishi Wao Na Wanafunzi  Ambayo Zoezi Hilo Linatakiwa Kufanywa Na Shule Zote Za Serikali Na Watu Binafsi.

Amesema Kuwa Mafunzo Yatakayo Tolewa Katika Semina Hiyo Wanatakiwa Kwenda Kuyatumia Vizuri   Na Kwenda Kusimamia Utekelezaji Wake  Wa Majukumu Huku Akisema Kuna Baadhi Ya Watendaji Wa Serikali Wamekuwa Kikwazo Kwa Walimu Na Kwamba  Wanatakiwa Kutoa Taarifa Kwa Viongozi Wa Ngazi Za Juu Kwa Wale Wanaowatishia Walimu Wakiwa Kazini.

Awali Akisoma Taarifa Fupi  Ya Mafunzo  Kwa Wakuu Wa Shule  Kuhusu Uongozi  Na Usimamizi  Wa Shule  Mkufunzi Kutoka Ademu Bi. Ester  Jonas Amesema Kuwa  Lengo La Mafunzo Hayo Ni   Kuwajengea Uwezo  Wakuu Wa Shule  Ili Kuimarisha Usimamizi Na Utendaji  Wa Elimu  Hususani Mpango Wa  Maendeleo  Ya Elimu  Ya Sekondari MMES 11.

No comments:

Post a Comment