Thursday, February 26, 2015
TASAF YAENDESHA SEMINA YA SIKU MBILI KWA WARATIBU WA MPANGO,WAHASIBU WA MPANGO,MAAFISA UFUATILIAJI, NA WAANDISHI WA HABARI KUTOKA MIKOA YA NJOMBE,MBEYA,IRINGA NA RUVUMA
MKURUGENZI MTENDAJI WA TASAF LADSLAUS MWAMANGA AKIZUNGUMZA WAKATI WA UFUNGUZI
WAJUMBE WA KIKAO KAZI KILICHOFANYIKA MJINI NJOMBE
Na Michael Ngilangwa
Mfuko Wa Maendeleo Ya Jamii (Tasaf) Umekiri Kuwepo Kwa Vyombo Vya Habari Nchini Ndiyo Msaada Mkubwa Katika Kuhamasisha Mpango Wa Kunusuru Kaya Maskini Kwa Kutumia Kalamu Zao Kuelimisha Wananchi Juu Ya Mpango Huo.
Mkurugenzi Mtendaji Wa Mfuko Wa Maendeleo Ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga Amesema Vyombo Vya Habari Ndiyo Vyenye Ushawishi Mkubwa Unaochangia Maendeleo Ya Wananchi Waliowengi Wa Mijini Na Vijijini.
Akifungua Semina Ya Siku Mbili Kwa Waratibu Wa Mpango, Wahasibu Wa Mpango, Maafisa Ufuatiliaji Na Waandishi Wa Habari Kutoka Mikoa Ya Mbeya, Njombe, Iringa Na Ruvuma, Iliofanyika Katika Ukumbi Wa Kyando Mjini Njombe Mwamanga Amesema TASAF Hivi Sasa Imeona Iimalishe Mkakati Wa Mpango Kazi Kwa Ajili Ya Vyombo Vya Habari Ili Kuhabarisha Sifa Na Vigezo Vya Kaya Maskini.
Mwamanga Amesema Toka Wameanza Kutekeleza Mpango Huo, Umekwenda Vizuri Ambapo Wamefikia Viwango Vya Kimataifa, Lakini Bado Kuna Dosari Kidogo Kwa Maana Uelewa Wa Watu Katika Ngazi Mbalimbali Bado Haujawa Mzuri Kwa Sababu Kuna Upotoshaji Wa Taarifa Zinazohusu Mpango Huo.
Mkurugenzi Huyo Mtendaji Wa Tasaf Amesema Inawezekana Wapo Wananchi Wachache Hawajapata Taarifa Kuhusiana Na Mpango Huo, Jambo Ambalo Wameona Hivi Sasa Waimalishe Mpango Mkakati Wa Kupashana Habari Kwa Kutumia Vyombo Mbalimbali Ambavyo Vipo Katika Maeneo Ya Utekelezaji.
Amesema Kuwa Katika Kuanza Ukurasa Mwingine Wa Kuboresha Ushirikiano Wanahabari Katika Maeneo Husika Na Watendaji Katika Shughuli Za Mpango Wanapaswa Kuwa Kitu Kimoja, Pasipo Kutafutana Ubaya Katika Utendaji, Badala Yake Wafanye Kazi Pamoja Kwa Kutumiza Malengo Ya Serikali.
Akizungumzia Umuhimu Wa Kutumia Waandishi Wa Habari Katika Mpango Wa Kunusuru Kaya Maskini Nchini, Amesema Ni Vyema Jamii Ikajitoa Kuwasaidia Wananchi Waliowengi.
Awali Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkurugenzi Wa Kuwajengea Uwezo Tasaf Bwana Fariji Mishael Amezuia Viongozi Wa Vijiji Kuwekwa Kwenye Mpango Wa Tasaf Kuwa Kama Wanufaika Kwenye Mpango Kwani Wao Wanauwezo Kupata Kipato Na Kuboresha Maisha Yao Kuliko Walengwa Ambao Ni Kaya Masikini Huku Akisema Wanahitaji Kushauriana Kwa Kushirikiana Na Wanahabari Hivyo Ni Lazima Kusisitiza Hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment