Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Ameziagiza Halmashauri Zote Za Mkoa Wa Njombe Kutenga Maeneo Ya Viwanja Kwaajili Ya Watumishi Wa Elimu Hususani Walimu Ikiwa Ni Pamoja Na Kuwajengea Nyumba Ili Watakapo Staafu Waweze Kuwa Na Sehemu Za Kuishi.
Dkt Nchimbio Ametoa Agizo Hilo Wakati Wa Ufunguzi Wa Semina Ya Siku Sita Kwa Wakuu Wa Shule Za Sekondari Za Serikali Na Za Watu Binafsi Kinachofanyikia Katika Ukumbi Wa Turbo Tangu Februari 23 Ambapo Semina Hiyo Imeandaliwa Na Watu Wa Ademu
Aidha Dkt Nchimbi Amesema Kuwa Ofisi Ya Mkoa Wa Njombe Inatarajia Kuandaa Tuzo Kwa Viongozi Wakuu Katika Sekta Ya Elimu Ambapo Amesema Hali Hiyo Itasaidia Kuwapa Motisha Na Moyo Wa Kufundisha Na Kuondoa Manung'uniko Miongoni Mwa Baadhi Ya Wakuu Hao.
Katika Hatua Nyingine Dkt Nchimbi Amewataka Wamiliki Wa Shule Za Watu Binafsi Kuwa Shirikisha Viongozi Wa Serikali Katika Kushirikiana Kutatua Baadhi Ya Changamoto Zinazowakabili Huku Wakitakiwa Kuweka Mazingira Rafiki Kwa Watumishi Wao Na Wanafunzi Ambayo Zoezi Hilo Linatakiwa Kufanywa Na Shule Zote Za Serikali Na Watu Binafsi.
Amesema Kuwa Mafunzo Yatakayo Tolewa Katika Semina Hiyo Wanatakiwa Kwenda Kuyatumia Vizuri Na Kwenda Kusimamia Utekelezaji Wake Wa Majukumu Huku Akisema Kuna Baadhi Ya Watendaji Wa Serikali Wamekuwa Kikwazo Kwa Walimu Na Kwamba Wanatakiwa Kutoa Taarifa Kwa Viongozi Wa Ngazi Za Juu Kwa Wale Wanaowatishia Walimu Wakiwa Kazini.
Awali Akisoma Taarifa Fupi Ya Mafunzo Kwa Wakuu Wa Shule Kuhusu Uongozi Na Usimamizi Wa Shule Mkufunzi Kutoka Ademu Bi. Ester Jonas Amesema Kuwa Lengo La Mafunzo Hayo Ni Kuwajengea Uwezo Wakuu Wa Shule Ili Kuimarisha Usimamizi Na Utendaji Wa Elimu Hususani Mpango Wa Maendeleo Ya Elimu Ya Sekondari MMES 11.
Semina Hiyo Imewahusisha Wakuu Wa Shule Za Sekondari Kutoka Mkoa Wa Mbeya Na Njombe Inatarajia Kuendeshwa Kwa Siku Sita Imedaiwa Itawasaidia Wakuu Wa Shule Hizo Kuboresha Kiwango Cha Taaluma Shuleni.
PICHA ZITAKUJIA HIVI PUNDE
No comments:
Post a Comment