Hatimaye Shule Ya Msingi Ujamaa Imeanza Kutoa Chakula Cha Mchana Kwa Wanafunzi Baada ya Afisa Elimu wa Shule za Msingi za Halmashauri ya Mji wa Njombe Zegeli Shengelo Kwenda Kufanya Mazungumza na Viongozi wa Shule na Mtaa huo Kuhusiana na Utoaji wa Chakula Hicho.
Hatua Hiyo Ya Afisa Elimu Wa Shule Za Msingi Wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Mwalimu Shengelo Imekuja Ikiwa Ni Siku Chache Baada Ya Kituo Cha Matangazo Cha Uplands Fm Radio Kuarifu Kuwa Shule Ya Msingi Ujamaa Haitoi Chakula Cha Mchana Kwa Muda Wa Wiki Mbili Kutokana Na Wazazi Kushindwa Kuchangia Chakula Hicho.
Wakizungumza Na Mtandao huu Baadhi Ya Wazazi Wenye Watoto Katika Shule Hiyo Wamesema Sababu Ya Kushindwa Kuchangia Chakula Cha Mchana Kwa Wanafunzi wa Shule Ya Msingi Ujamaa Ni kutokana Na Mgongano Wa Kimaslahi Kwa Baadhi Ya Viongozi Wa Mtaa Na Kamati Ya Chakula Kushindwa Kuaminiana Katika Ukusanyaji Wa Chakula Kwa Wazazi.
Akizungumza ofisini kwake Mwenyekiti Wa Kamati Ya Chakula Katika Shule Ya Msingi Ujamaa Bwana Winfred Kayombo Amekili Shule Hiyo Kuanza Kutoa Chakula Cha Mchana Baada Ya Afisa Elimu Wa Shule Za Msingi Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Kuzungumza Nao Na Kufikia Uamuzi Wa Wazazi Kuanza Kuchangia Chakula Hicho Ambacho Kinaendelea Kuchangiwa Hadi Sasa.
Afisa Mtendaji Wa Mtaa Wa Kibena Hospitali Bi.Kolumba Msemwa Amesema Jitihada Za Serikali Ya Mtaa Huo Zimeendelea Kufanyika Baada Ya Afisa Elimu Zegeli Shengelo Kutoa Agizo La kutolewa Chakula Hicho Ambapo Serikali Ya Mtaa Huo imeamua Kuwafuata Na Askali Mgambo Baadhi ya Wazazi Wasiyopenda Kuchangia Chakula Hicho Na Kwamba Kwa Watakaoshindwa Watafikishwa Katika Vyombo Vya Sheria.
No comments:
Post a Comment