Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, November 18, 2014

RC NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI AAGIZA HALMASHAURI KUPIMWA NA KUWEKA MIPAKA YA SHULE ILI KUONDOA MIGOGORO BAINA YA WANANCHI WA VIJIJI NA SHULE ZAO


  MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI  AWAASA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI WAEPUKANA NA VISHAWISHI.
 
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dokta Rehema Nchimbi Ameiagiza Halmashauri ya Mji wa Njombe Kuhakikisha Inapima na Kuweka Mipaka Katika Shule Zote za Msingi na Sekondari Ili Kuepusha Uvamizi wa Maeneo ya Shule Hizo.

Dokta Nchimbi Ametoa Agizo Hilo Akiwa Mgeni Rasmi Katika Mahafali ya Kwanza ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Anne Makinda na Kwamba Uvamizi wa Maeneo ya Shule Utatatuliwa Kwa Kupimwa na Kuwekwa Mipaka Ndani ya Maeneo Hayo.

Katika Hatua Nyingine Mkuu Huyo wa Mkoa Amesisitiza Juu ya Utekelezaji wa Agizo la Rais Profesa Jakaya Kikwete Katika Ujenzi wa Maabara Tatu Kwa Kila Shule ya Sekondari Hadi Ifikapo Novemba 30 Mwaka Huu.

Pia Ametumia Fursa Hiyo Kuwaagiza Wakuu wa Wilaya Zote za Mkoa wa Njombe Kuhakikisha Wanawachukulia Hatua za Kisheria Wazazi na Walezi wa Wanafunzi wa Kike Wanaowakatisha Masomo Watoto Wao  Kwa Kuwaozesha Angali Wadogo.

Sanjari na Hilo Lakini Pia Amewataka Watoto Wa Kike Katika Shule Hiyo Kuepuakana na Vishawishi na Anasa za Dunia Zinazoweza Kuwaharibia Masomo na Ndoto za Maisha Yao ya Baadaye.

Akikagua Maendeleo ya Ujenzi wa Maabara Katika Shule Hiyo Dokta Nchimbi Amepongeza Hatua Kubwa Iliyofikiwa Katika Ujenzi Huo Licha ya Kuwa Bado Wanafunzi Katika Shule Hiyo Wanaendelea Kupata Mazoezi Kwa Vitendo Kwa Kutenga Vyumba Maalumu Kwa Ajili ya Masomo ya Sayansi Huku akiagiza Ufugaji wa Nyuki kwaajili ya Walimu.

Taarifa ya Shule Hiyo Iliyosomwa na Mkuu wa Shule Hiyo Bi. Velonica Mlozi Amesema Jumla ya Wanafunzi 79 wa Kike Wametunukiwa Vyeti Vya Kuhitimu Masomo ya Kidato Cha Nne Kwa Mwaka Huu Huku Shule Hiyo Ikikabiliwa na Changamoto Mbalimbali Ikiwemo Uhaba wa Nyumba za Walimu,Huduma ya Nishati ya Umeme Pamoja na Ukosefu wa Walimu wa Masomo ya Sayansi.

No comments:

Post a Comment