Makamu
wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali (watatu kutoka kulia) akiwa kwenye
picha ya pamoja na wadau wa Sekta ya afya nchini mara baada ya kufungua
Kongamano la wadau hao leo jijini Dar es salaam.Wengine kushoto ni
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid.Picha zote na Frank Mvungi-MAELEZO_Dar es salaam.
Makamu
wa Rais Dk. Mohemed Gharib Bilali akiwa kwenye picha ya pamoja na
Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid leo Jijini Dar es
salaam wakati wa Kongamano la wadau wa Sekta ya Afya lililofanyika leo
Jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya Wadau wa Kongamano la wadau wa Sekta ya Afya wakiwa wanamsikiliza
mgeni rasmi ambaye ni makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali (hayupo
pichani) wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo leo jijini Dar es salaam.
…………………………………
…………………….
Na Frank Mvungi-MAELEZO
Serikali imesema itaendelea kuboresha huduma za afya hapa nchini kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hosipitali za Rufaa zote nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata matatibu bora na yanayoridhisha.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilali wakati akifungua Kongamano la wadau wa Afya nchini.
Serikali imesema itaendelea kuboresha huduma za afya hapa nchini kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hosipitali za Rufaa zote nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata matatibu bora na yanayoridhisha.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilali wakati akifungua Kongamano la wadau wa Afya nchini.
Amesema kuwa Serikali inayo dhamira ya dhati katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata huduma bora za afya ili apate muda mzuri wa kuchangia shughuli nyingine za maendeleo akiwa mzima.
Dkt. Bilali ameongeza kuwa Serikali itaendelea kutoa motisha kwa watumishi wa Sekta ya afya ili waendelee kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.
Kwa upande wake Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid amesema Tanzania ni moja kati ya nchi nne barani Afrika zilizoweza kufikia lengo namba 4 la malengo ya millennia katika utoaji wa huduma bora za afya.
Amesema kuwa hatua imefikiwa baada ya Wizara hiyo kuamua kuanzisha idara maalum itakayohusika kuangalia ubora wa huduma zinazotolewa hapa nchini ili kuongeza tija katika Sekta ya Afya kwa kuwapa Wananchi huduma bora zinazokidhi vigezo.
Ameongeza kuwa kwa wale wanaofanya vizuri katika kutoa huduma za Afya watatambuliwa kwa mchango wao katika kutoa huduma bora. Dkt.
Rashid ametaja vigezo vinavyotumika katika kuwapata watoa huduma za
afya kuwa ni kutoa huduma inavyotakiwa,kutumia utaalamu sahihi katika
kutoa huduma hiyo na kuzingatia viwango vilivyowekwa katika kutoa huduma
za afya.
Aidha
Dkt. Rashid ametoa wito kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya(NHIF) ili waweze kunufaika na huduma zinazotolewa kupitia mfuko
huo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora za
afya. Kongamano
la wadau wa Sekta ya Afya limehusisha wadau zaidi ya 300 kutoka katika
Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Kiserikali na linafanyika
kwa muda wa siku mbili ambapo baadhi ya wadau walitambuliwa kwa kutoa
huduma bora za Afya ni kama vile Hosipitali ya Rufaa Mbeya,KCMC, na
Bugando.
No comments:
Post a Comment