Mtangazaji
wa zamani wa Radio Tanzania (RTD) sasa TBC,Ben Hamis Kikoromo maarufu
kama Ben Kiko enzi za uhai wake akiwa katika moja ya semina
alizohudhuria.
MTANGAZAJI
na mwandishi wa habari mkongwe nchini Ben Kiko amefariki dunia usiku wa
kuamkia leo katika hosptali ya taifa ya rufaa ya Muhimbili jijini Dar
es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Ben
Kiko ambaye jina lake kamili ni Ben Hamisi Kikoromo alihamishiwa katika
hosptali ya Muhimbili kutokea hosptali ya Jeshi ya Milambo ya mkoani
Tabora ambako alilazwa kwa ajili ya matibabu ya figo kwa muda wa wiki
mbili.
MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA,
AMIN
|
Mtangazaji
wa zamani wa Radio Tanzania (RTD) sasa TBC, Ben Hamis Kikoromo maarufu
kama Ben Kikoakizungumza na Mwakilishi wa Globu ya Jamii Kanda ya
Kaskazini Dixon Busagaga alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Cheyo
mkoani Tabora wakati wa uhai wake.
|
Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania Dar es salaam ambayo sasa ni TBC Taifa, Ben Hamis Kikoromo (pichani akiwa ameshika hati ya Tuzo ya Utumishi uliotukuka wa Maisha April 2012) maarufu kama Ben Kiko,
atakumbukwa
kama mmoja wa watangazaji mahiri ambao walijipatia umaarufu mkubwa
ambapo katika enzi za uhai wake alifanya makubwa wakati wa Vita vya
Kagera kwa kuleta matukio mbalimbali kutoka uwanja wa vita. Pia
aliupaisha sana mkoa wa Tabora alikokuwa akifanyia kazi kwa habari na
visa mbalimbali katika kipindi cha RTD cha Majira.
No comments:
Post a Comment