“Nimeshtushwa na kusikitishwa sana kutokana na ajali hii mbaya ambayo kwa ghafla imeondoa uhai wa wenzetu 12 wasio na hatia kutokana na kukosekana kwa umakini wa binadamu katika uendeshaji wa vyombo vya moto katika barabara zetu”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake.
Ameongeza Rais Kikwete: “Kutokana na ajali hiyo, naomba upokee Salamu zangu za Rambirambi, na kupitia kwako, Salamu hizi na pole nyingi ziwafikie wafiwa wote kwa kupotelewa ghafla na wapendwa wao. Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema azipokee na kuzilaza Roho za Marehemu wote mahala pema peponi, Amina”.
Aidha, Rais Kikwete amewapa pole sana wote walioumia katika ajali hiyo akimwomba Mwenyezi Mungu awape ahueni ili wapone haraka na kuweza kurejea katika shughuli za maendeleo yao na yale ya taifa. “Naomba Mwenyezi Mungu awajalie ahueni ya haraka, ili muweze kupona haraka na kurejea katika maisha yenu ya kujitafutia riziki na kuchangia maendeleo ya taifa letu.”
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
31 Oktoba,2014
No comments:
Post a Comment