Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, November 1, 2014

MWILI WA MEJA JENERALI AIDAN ISIDORI MFUSE UNATARAJIA KUZIKWA KESHO KATIKA MAKABURI YA MPECHI MJINI NJOMBE

Marehemu Meja Jenerali (mst.) Aidan Isidore Mfuse 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange anasikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) kilichotokea tarehe 29 Oktoba 2014 katika Hospitali ya Appolo nchini
India alikokuwa akipata matibabu.
Mwili wa marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) unatarajia kuwasili Tanzania tarehe 31 Oktoba 2014 saa 7:30 mchana na kuhifadhiwa katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo. Heshima za mwisho kwa Viongozi, Wanajeshi na Watumishi wa Umma zitatolewa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo tarehe 01 Novemba 2014, kuanzia saa
4.00 hadi saa 5.00 asubuhi na mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Njombe kwa mazishi, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika tarehe  02 Novemba, 2014 saa 8.00 mchana.  

Imetolewa  na  Kurugenzi  ya
Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 - 309963

No comments:

Post a Comment