Friday, October 10, 2014
NJOMBE HIGH SCHOOL YALAZIMIKA KUFUNGA KWA MWEZI MMOJA KUPISHA UCHUNGUZI WA KUBAINI WALIOHUSIKA KUCHOIMA BWENI NA KUHARIBU MALI
HAWA NI WANAFUNZI WA NJOMBE SEKONDARI WAKIPEWA ADHABU ILI WATAJE WALIOHUSIKA NA UCHOMAJI MOTO NA UHARIBIFU HUO WA MALI
WANAFUNZI WA SHULE YA NJOMBE SEKONDARI WAKILISHWA PUSHAPU ILI WASEMA MUHUSIKA WA UCHOMAJI NA UHARIBIFU HUO
AFISA ELIMU MKOA WA NJOMBE AKIFUNGA KWA NIABA YA KAMISHNA WA ELIMU NCHINI SAID KINYAGA NYASIRO
WANAFUNZI WA NJOSS WAKIWA KATIKAUWANJA WA PARAD GROUND WAKATI MAAMUZI YA KIUFUNGA KWA SHULE HIYO YAKITOLEWA
SOMA UBAONI HAPO MAANDISHI YALIVYOANDIKWA INASADIKIKA NI VIJANA HAO WAKIWA SHULE YA MSINGI KILIMANI NJOMBE
Na Michael Ngilangwa-Njombe
Shule Ya Sekondari Njombe Imelazimika Kufunga Kwa Muda Wa Mwezi Mmoja Kufuatia Wanafunzi Wa Shule Hiyo Kuteketeza Kwa moto jengo la Bweni Namba Nane,Jengo La Kalakana Na Kuharibu Mali Nyingene Za Shule Hiyo Pamoja Na Shule Ya Msingi Kilimani Ili Kupisha Uchanguzi Wa Tukio Hilo.
Akizungumza Kwa Niaba Ya Kamishna Wa Elimu Nchini,Afisa Elimu Wa Mkoa Wa Njombe Said Nyasiro Amesema Kuwa Zaidi Ya Shilingi Milioni Mia Moja Arobaini Na Moja Na Laki Moja Na Tisini Elfu Ambapo Kwa Upande Wa Mali Za Shule Zilizoteketezwa Kwa Moto Zimegharimu Zaidi Ya Shilingi Milioni Mia Moja.
Aidha Afisa Elimu Mwalimu Nyasiro Amesema Kuwa Shule Hiyo Imefungwa Hadi Tarehe
Nane Mwezi Wa Kumi Na Moja Ambapo Mwanafunzi Anatakiwa Kurudi Na Mzazi Wake
Akiwa Na Fedha Tasilimu Shilingi Laki Moja Na Nusu Kwaajili Ya Kufidia Sehemu
Zilizoharibiwa Na Wanafunzi Hao.
Akibainisha Baadhi Ya Mali Zilizoharibiwa Na Wanafunzi Hao Said Nyasiro Ni Pamoja na Bweni La Shule Litagharimu Shilingi Milioni Mia Moja, Uharibifu katika Shule Ya Msingi Kilimani Shilingi Laki Tatu Na Hamsini,Vifaa Vya Wanafunzi Vilivyoungua Zaidi ya Shilingi Milioni Ishilini Na Nane Na Mia Sita Arobaini,Uharibisha Wa Nyumba Ya Mwalimu Laki Tano,Kalakana ya shule Milioni Kumi,Duka La Mwalimu Milioni Moja Vyenye Zaidi Ya Shilingi Milioni Mia Moja Arobaini Na Moja.
Kwa Upande Wake Mkuu Wa Shule Ya Sekondari Njombe Benald William Akizungumzia
Chanzo Cha Hatua Ya Wanafunzi Hao Kuharibu Mali Za Shule Na Kuchoma Misitu Na Bweni Namba Nane,Kuharibu Vioo Vya Madirisha Na Mali Mbalimbali Za Shule, Walimu Pamoja Na Shule Ya Msingi Kilimani Bado Hakijafahamika.
Amesema Tukio Hilo Huenda Likahusishwa Na Baadhi Ya Wanafunzi Waliorudishwa
Nyumbani Baada Ya Bodi Ya Shule Kukutana October 7 Shuleni Hapo Na Kujadili Baadhi Ya Wanafunzi Waliotoroka Na Kwenda Disco Chuo Cha Maendeleo Njombe Pasipo Ruhusa Ya Walimu Na Ni Kwa Nyakati Za Usiku Na Kusababisha Mmoja Wao Kuvunjika Mguu Ambapo Uchunguzi Zaidi Bado Unaendelea.
Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Linawashikilia Baadhi Ya Wanafunzi Ambao Wanahisiwa Kuhusika Na Tukio Hilo Kwa Uchunguzi Zaidi Ambapo Shule Ya Wavulana Wa Sekondari
Njombe Ina Jumla Ya Wanafunzi Mia 987 Wa Kidato Cha Tano Na Cha Sita Iliyowekewa Jiwe La Msingi Na Rais Wa Awamu Ya Kwanza Hayati Julius Kambalage Nyerere Mwaka Mwaka 1973.
Kufuatia kutokea tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linaendelea na Mahojiano na Wanafunzi 15 wa Shule ya Sekondari NJOMBE[NJOSS] Baada ya Kufanya Vurugu Kubwa na Kusababisha Uhalibifu wa Mali Mbalimbali za Shule Hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa Njombe SACP Fulgency Ngonyani Amesema Kuwa Wanafunzi Hao 15 ni Miongoni Mwa Walioonekana Kuhusika Moja Kwa Moja Katika Vurugu Hizo na Kwamba Baadhi yao Wameachiwa Baada ya Kujiridhisha Kuwa Hawakuhusika na Tukio Hilo.
Kamanda Ngonyani Amewataja Wanafunzi Wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi Kwa Mahojiano Zaidi Kuwa ni Pamoja na Johnson Mbelele,Ndanga Obadia na Ezra Charles Kama Hapa Anavyowataja.
Kutokana na Uhalibifu Huo Mkubwa wa Mali za Umma Uliosababishwa na Wanafunzi Hao Ambao Wanadaiwa Kufanya Vurugu Hizo Kufuatia Wenzao 29 Kusimamishwa Masomo Kwa Utovu wa Nidhamu Kwa Kutoroka Kwenda Disko Katika Chuo Cha Maendeleo Amewataka Wanafunzi Hao Kutumia Njia Mbadala Kwa Kuwashirikisha Viongozi Wengine Nje ya Shule Pindi Wanapopatwa na Matatizo.
Aidha Amesema Kuwa Kufanya Vurugu na Kuharibu Mali za Shule ni Kinyume Cha Sheria na Hivyo Mahojiano Zaidi Yanaendelea Ambapo Baada ya Upelelezi Kukamilika Watafikishwa Mahakamani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment