Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, October 9, 2014

KAMISHNA WA ELIMU NCHINI ALAZIMIKA KUFUNGA SHULE YA SEKONDARI NJOMBE {NJOSS} KWA KIPINDI CHA MWEZI MMOJA KUFUATIA KUTEKETEZWA KWA BWENI NA KUHARIBIWA MALI MBALIMBALI ZA SHULE HIYO

 HILI NI BWENI LILILOCHOMWA MOTO JANA KATIKA SHULE HIYO























































 KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE SACP FULGENCE NGONYANI AKIKAGUA UHARIBIFU ULIOTOKEA KWA KUCHOMWA MOTO NA KUVUNJWA  KWA MADIRISHA


 HAWA NDIYO WAMEPELEKWA KITUONI KWA MAHOJIANO ZAIDI


 BAADHI YA WANAFUNZI WAKIPAKIWA KWENYE GARI LA POLISI NA KUPELEKWA KITUONI





 BAADHI YA WANAFUNZI WA NJOMBE SEKONDARI WAKIWA WAMEMBEBA MWENZAO ALIYEVUNJIKA MGUU






 WANAFUNZI WA SHULE YA NJOMBE SEKONDARI WAKILISHWA PUSHAPU ILI WASEMA MUHUSIKA WA UCHOMAJI NA UHARIBIFU HUO







 AFISA ELIMU MKOA WA NJOMBE AKIFUNGA KWA NIABA YA KAMISHNA WA ELIMU NCHINI SAID  KINYAGA NYASIRO

 WANAFUNZI WA NJOSS WAKIWA KATIKAUWANJA WA PARAD GROUND WAKATI MAAMUZI YA KIUFUNGA KWA SHULE HIYO YAKITOLEWA






Shule Ya Sekondari Njombe  Imelazimika Kufunga Kwa Muda Wa Mwezi  Mmoja Kufuatia  Wanafunzi Wa Shule Hiyo Kuteketeza  Kwa moto jengo la  Bweni Namba Nane,Jengo La Kalakana  Na  Kuharibu Mali Nyingene Za Shule Hiyo Pamoja Na Shule Ya Msingi Kilimani  Ili Kupisha  Uchanguzi Wa Tukio Hilo.

Akizungumza Kwa Niaba Ya Kamishna Wa Elimu Nchini,Afisa Elimu Wa Mkoa Wa Njombe  Said Nyasiro Amesema Kuwa  Zaidi Ya Shilingi Milioni  Mia Moja Arobaini Na Moja Na Laki  Moja Na  Tisini  Elfu Ambapo Kwa Upande Wa Mali Za Shule Zilizoteketezwa Kwa Moto  Zimegharimu Zaidi Ya Shilingi Milioni Mia Moja.

Aidha Afisa Elimu Mwalimu Nyasiro Amesema Kuwa Shule Hiyo Imefungwa Hadi Tarehe 
Nane Mwezi Wa Kumi Na Moja  Ambapo Mwanafunzi Anatakiwa Kurudi Na Mzazi Wake 
Akiwa Na Fedha Tasilimu Shilingi Laki Moja Na Nusu Kwaajili Ya Kufidia Sehemu 
Zilizoharibiwa Na Wanafunzi Hao.

Akibainisha Baadhi Ya Mali Zilizoharibiwa  Na Wanafunzi  Hao   Said  Nyasiro Ni Pamoja na  Bweni La Shule  Litagharimu Shilingi Milioni Mia Moja, Uharibifu katika Shule Ya  Msingi Kilimani  Shilingi Laki Tatu Na Hamsini,Vifaa Vya Wanafunzi Vilivyoungua   Zaidi ya Shilingi Milioni Ishilini Na Nane Na Mia Sita Arobaini,Uharibisha Wa  Nyumba Ya Mwalimu Laki Tano,Kalakana ya shule   Milioni Kumi,Duka La Mwalimu Milioni  Moja Vyenye   Zaidi Ya  Shilingi Milioni Mia Moja Arobaini Na Moja.

Kwa Upande Wake  Mkuu Wa Shule Ya Sekondari Njombe  Benald William Akizungumzia 
Chanzo Cha Hatua Ya Wanafunzi Hao Kuharibu Mali Za Shule Na Kuchoma Misitu Na Bweni  Namba Nane,Kuharibu Vioo Vya Madirisha Na Mali Mbalimbali Za Shule, Walimu Pamoja Na   Shule Ya Msingi Kilimani Bado Hakijafahamika.

Amesema Tukio Hilo Huenda Likahusishwa Na Baadhi Ya Wanafunzi Waliorudishwa 
Nyumbani Baada Ya Bodi Ya Shule Kukutana October 7 Shuleni Hapo Na Kujadili Baadhi Ya  Wanafunzi Waliotoroka  Na Kwenda Disco  Chuo Cha Maendeleo Njombe Pasipo Ruhusa Ya  Walimu Na Ni Kwa Nyakati Za Usiku Na Kusababisha Mmoja Wao Kuvunjika Mguu  Ambapo  Uchunguzi Zaidi Bado Unaendelea.

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Linawashikilia Baadhi Ya Wanafunzi Ambao Wanahisiwa  Kuhusika Na Tukio Hilo Kwa Uchunguzi Zaidi Ambapo Shule Ya Wavulana Wa Sekondari 
Njombe  Ina Jumla Ya Wanafunzi Mia 987  Wa Kidato Cha Tano Na Cha Sita Iliyowekewa Jiwe  La Msingi Na Rais Wa Awamu Ya Kwanza Hayati Julius Kambalage Nyerere Mwaka  Mwaka  1973.

Kufuatia kutokea tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linaendelea na Mahojiano na Wanafunzi 15 wa Shule ya Sekondari NJOMBE[NJOSS] Baada ya Kufanya Vurugu Kubwa na Kusababisha Uhalibifu wa Mali Mbalimbali za Shule Hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa Njombe SACP Fulgency Ngonyani Amesema Kuwa Wanafunzi Hao 15 ni Miongoni Mwa Walioonekana Kuhusika Moja Kwa Moja  Katika Vurugu Hizo na Kwamba Baadhi yao Wameachiwa Baada ya Kujiridhisha Kuwa Hawakuhusika na Tukio Hilo.

Kamanda Ngonyani Amewataja Wanafunzi  Wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi Kwa Mahojiano Zaidi Kuwa ni Pamoja na Johnson Mbelele,Ndanga Obadia na Ezra Charles Kama Hapa Anavyowataja.

Kutokana na Uhalibifu Huo Mkubwa wa Mali za Umma Uliosababishwa na Wanafunzi Hao Ambao Wanadaiwa Kufanya Vurugu Hizo Kufuatia Wenzao 29 Kusimamishwa Masomo Kwa Utovu wa Nidhamu Kwa Kutoroka Kwenda Disko Katika Chuo Cha Maendeleo Amewataka Wanafunzi Hao Kutumia Njia Mbadala  Kwa Kuwashirikisha Viongozi Wengine Nje ya Shule Pindi Wanapopatwa na Matatizo.


Aidha Amesema Kuwa Kufanya Vurugu na Kuharibu Mali za Shule ni Kinyume Cha Sheria  na Hivyo Mahojiano Zaidi Yanaendelea Ambapo Baada ya Upelelezi Kukamilika Watafikishwa Mahakamani.


No comments:

Post a Comment