Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, October 31, 2014

MADIWANI WATAKIWA KUHAMASISHA WANANCHI KWENYE SHUGHULI ZA MAENDELEO. .


Meza kuu ikifuatilia Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gulam Hussein Kiffu, Mkurugenzi Adam Mgoyi na Makamu Mwenyekiti wa HalmashauriGulzar Sabil.

.Madiwani wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiendelea katika mkutano wa Baraza la Madiwani Mbarali.

 Wakuu wa Idara mbali mbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Madiwani.


Baraza zima la Madiwani pamoja na wakuu wa Idara wakiendelea na Mkutano

MKUU wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Gulam Hussein Kiffu, amewataka Madiwani kusaidiana na Watendaji wa Kata na Vijiji kuwahamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa Maabala unaondelea wilayani humo.
Wito huo aliutoa katika Mkutano wa kwanza wa mwaka wa fedha 2014/2015 wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Maji uliopo Rujewa.
Kiffu alisema licha ya  uwepo wa kasi nzuri ya ujenzi wa Maabara katika shule za Sekondari wilayani humo ni vema Madiwani wakaendelea kuwahamasisha Wananchi wakishirikiana na Watendaji kuchangisha fedha za umaliziaji wa majengo hayo.
Alisema ni matumaini yake kuwa ifikapo mwezi Novemba zoezi hilo likawa limekamilika kwa kiwango kikubwa na kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kufanya ziara ya kukagua majengo hayo tayari kwa kuanza kuyatumia.
Alisema uwepo wa Maabara katika shule za Sekondari kutasaidia upatikanaji wa wataalamu wa masomo ya sayansi kutokana na kuandaliwa kuanzia ngazi ya chini kwa vitendo hali itakayowasaidia kuwaimarisha na kuwahamasisha wanafunzi kuyapenda masomo ya sayansi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Adam Kingoyi, alisema ni vema wanasiasa wakasaidia kuhamasisha shughuli za maendeleo katika maeneo yao na sio kukwamisha wakihofia kunyimwa kura katika uchaguzi ujao.
Mwisho.

Na Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment