Waandamanaji wakilitazama bunge
la Burkina Faso likiteketea kwa moto.
Magari nayo yameteketezwa kwa moto.
WAANDAMANAJI nchini
Burkina Faso leo wamechoma moto bunge la nchi hiyo kupinga kupitishwa
kwa katiba itakayomruhusu rais wa nchi hiyo, Blaise Compaore kuongeza
muda wa kukaa madarakani.
Rais Compaore anataka
kuongeza muda zaidi katika utawala wake wa miaka 27 aliyotumia
kuliongoza taifa hilo.
Taarifa kutoka Mji Kuu
ya nchi hiyo, Ouagadougou, zinasema kuwa ukumbi wa chama tawala na
makao makuu ya chama hicho cha Congress for Democracy and Progress
yamechomwa moto pia.
Bunge hilo lilitaka
kubadili katiba itakayomuwezesha Compaore, aliyeingia madarakani tangu
mwaka 1987 ili aweze kuiongoza tena nchi hiyo mwakani.
Kumekuwepo kampeni za
wapinzani wanaomtaka rais huyo kuachia ngazi na kutogombea katika
uchaguzi wa mwaka ujao.
Kabla ya kuchomwa moto
bunge hilo, polisi walilipua mabomu ya machozi kuwazuia waandamanaji
waliokuwa wakielekea katika jengo la bunge hilo japo takribani watu
1,500 walifanikiwa kupenya na kulichoma bunge hilo.
Waandamanaji
walionekana wakichoma nyaraka na kupora baadhi ya vifaa vya kompyuta
huku magari yaliyokuwa nje ya jengo hilo nayo yakichomwa moto.
No comments:
Post a Comment