KAMANDA WA POLISI MKOA WA NJOMBE SACP FULGENCE NGONYANI AKIWA OFISINI KWAKE
Na Michael Ngilangwa
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limewachisha Kazi Askali wake Watatu Ambao Ni Askali wenye namba G. 3172 PC Ramadhani Idd Said, G. 9693 PC Emmanuel Morson Lyimo Na Namba H. 2672 PC Miraji Jumanne Mtea Kwa Kosa la Utomvu wa Nidhamu likiwemo la Kupigana Hadharani.
Akizungumza na Uplands fm radio Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani Amesema hatua ya Jeshi hilo kuwafukuza kazi Askali hao imetokana na kujihusisha na Matukio maovu Kinyume na Mwendo Wa Jeshi hilo Ikiwemo tukio la hivi karibu la Kupigana Hadharani lililotokea October 24 mwaka huu.
Kamanda Ngonyani Amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Limeamua Kutoa Adhabu hiyo Ili kuwa Fundisho Kwa Watumishi Wengine Ambapo Pamoja Na Mambo Mengine Limewataka Wananchi Na Viongozi Mkoani hapa Kutoa Taarifa mapema kwa viongozi husika Pindi Watakapo Waona Askali hao wanaendelea na Kazi ya Kiaskali.
Katika Hatua Nyingine Jeshi Polisi Mkoani Hapa Linamshikilia Mkazi Mmoja wa Mlangali Keneth Mwakila Mwenye Umri Wa Miaka 52 Kwa Tuhuma za Kupatikana Na Dawa Za Kulevya Gramu 200 Aina ya Bangi Ambazo zilikutwa Kibandani kwake wakati wa Msako ulioendeshwa Hivi Karibuni.
SACP Fulgence Ngonyani Amesema Jeshi Hilo bado Linaendelea Na Msako Wa Kuwapata Waliohusika na Tukio la Kuvunja Na Kuiba Pikipiki Namba T 985 CBU Aina Ya T BETTER yenye Thamani ya Shilingi Milioni Moja na Laki saba Mali ya Bwana Rameck Nombo Mkazi wa Mtaa wa Ruhuji Ambayo Iliibiwa Mnamo October 25 Mwaka Huu.
No comments:
Post a Comment