Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, October 28, 2014

MAHAKAMA YA WILAYA YAWASOMEA MASHTAKA WASHTAKIWA WA MAKOSA YA MAUAJI KWAAJILI YA KESI ZAO KUSIKILIZWA NA MAHAKAMA KUU


Mahakama Ya Wilaya Ya Njombe Leo Imewasomea  Mashtaka Washtakiwa Mbalimbali Wa  Makosa Ya Mauaji  Kwaajili Ya Kesi Zao Kupelekwa Kusikilizwa Katika Mahakama Kuu   Ambapo Miongoni Mwa Washtakiwa Ni Pamoja Na Jason Swale Mkazi Wa Kijiji Cha 
Makolango Makambako Anayeshtakiwa Kwa Kosa La Kumuua Anastanzia Mangula.

Washtakiwa Wengine Ni Pamoja Na Jofrey Nyava Ambaye Anatuhumiwa Kumuua  Baba 
Yake Joshuwa Nyave Mkazi Wa Kijiji Cha Igwachanya,James Msumule Maarufu Kwa Jina La  Jembe,Emmanuel Ngairo Maarufu Kwa Jina  La Emma,Isack Ngairo,Anitha Mbwilo;Upendo  Mligo Ambao Wote Kwa Pamoja Wanatuhumiwa Kwa Kosa La Kumuua Alice Mtokoma   Mkazi Wa Kijiji Cha Usalule Wilayani Wanging'ombe.

Akisoma Hati Ya Mashtaka Na Maelezo Ya Mashahidi Watakaokwenda Kutolea Ushahidi Wao  Na Vielelezo Katika Mahakama Kuu, Wakili Wa Serikali  Riziki Matiku  Ameiambia Mahakama Kuwa    Mshtakiwa Geofrey Nyave Alitenda Kosa Hilo Mnamo April  Mwaka 2012 Ambapo Alifanya  Kosa La Mauaji Ya Kukusudia Kumuua Baba Yake Joshuwa Nyave Kinyume Na Kifungu Cha  196 Na 197 Cha Sheria Ya Kanuni Za Adhabu Sura Ya  16 Ya Marejeo Ya Mwaka 2002.

Wakili Matiku Amewataja Watuhumiwa  James Msumule,Emmanuel Ngairo,Isack 
Ngairo,Anitha Mbwilo Na Upendo Mligo Wakazi Wa Kijiji Cha Usalule Kuwa Walitenda Kosa  Hilo Kwa Kumuua Alice Mtokoma  Wakimutuhumu Kwa Imani Za Kishirikina Kinyume Na  Kifungu Cha 196 Na 197 Cha Sheria Ya Kanuni Ya Adhabu Sura Ya 16 Ya Marejeo Ya Mwaka  2002.

Aidha Wakili Matiku Amemtaja Mtuhumiwa Castori Chatanda  Mkazi Wa Kijiji Cha Iboya 
Kuhusika Na Mauaji Ya   Marehemu  Sebastian Chatanda Yaliotokea  July 2013 Kuwa Ni 
Mauaji Ya Kutokukusudia  Kinyume Na Kifungu Cha 195 Na 198  Sura Ya 16  Ilivyofanyiwa 
Marekebisho  Mwaka 2002.

Hakimu Wa Mahakama Ya Wilaya Ya Njombe Augustine Rwizile  Amesema Washtakiwa 
Hawaruhusiwi Kujibu Chochote Dhidi Ya Makosa Hayo Hadi Hapo Mashtaka Hayo Yatakapo  Fikishwa Katika Mahakama Kuu.

No comments:

Post a Comment