KWA HISANI YA FRANCIS GODWIN -IRINGA
Baadhi ya walinzi wa kampuni ya kiwango security guards Ltd wakiwa katika ofisi za TUPSE kannda ya nyanda za juu kusini leo kudai mishahara ya miezi miwili
ZAIDI ya
walinzi 60 wa Kampuni ya Kiwango Security Guards Ltd kanda ya Iringa
wamegoma kuendelea na kazi ya kulinda minara ya Vodacom wakidai
mishahara ya miezi miwili kutoka kwa mwajiri.
Walinzi
hao kutoka sehemu mbalimbali ya mkoa wa iringa wakiongea na MATUKIO DAIMA
leo kwa machungu katika ofisi za Chama cha Wafanyakazi Walinzi Binafsi
Tanzania (TUPSE) Kanda Nyanda za juu Kusini zilizopo mjini Iringa,
walisema kuwa wana muomba Rais Jakaya Kikwete awasaidie kutatua tatizo
la mwajiri wao ili awalipe mishahara yao ya miezi miwili wanayomdai.
"Mwajiri
huyo ni wa kampuni ya ulinzi ya kiwango kutoka jijini Dar es salaam
hajatulipa mishahara yetu,kwa kweli hali ni nguu kweli sasa sisi
tunafanya kazi kama nyuki tunatumikishwa na hadi sasa tuna miezi miwili
hatujalipwa na tunafamilia hatujui familia zetu zitaishi hivyo
tunamuomba rais aingilie kati ili tuweze kulipwa mishahara
yetu.'walisema
Mzee
Ismaili Mpenge (68) ambaye analinda mnara wa Vodacom kadeti uliopo
kijiji cha Nyang'oro katika jimbo la isimani iringa alisema kampuni hiyo
haijamlipa mishahara ya miezi miwili tangu aanze kazi Julai nne mwaka
huu.
Alisema
kuwa tangu jana afike mjini iringa kutoka kijijini kwake hajala na nauli
yakufika mjini amekopa na kuongeza kuwa hapa mjini hana ndugu na kuomba
wasamaria wema wamsaidie sehemu ya kulala anaposubiria malipo.
"Nimetoka
katika kijiji cha Nyang'oro tangu jana na sijui hatma na isitoshe tuna
watoto wanasoma na mpaka sasa hatujui familia zetu zinakula nini mpaka
sasa ... kwa kweli maisha yetu walinzi ni magumu," alisema.
Naye
Isaya Mdabagi mlinzi wa mnara wa migori alisema kuwa kwa miezi miwili
hatujalipwa mishahara ukizingatia tuna familia tulizoziacha huku
nyumbani bila chochote.
Mwajiri
aliahidi kulipa mshahara wa mwezi moja na sio mshahara wote kama
makubaliano yetu ya kulipwa laki na ishirini lakini amesema kuwa
watalipwa shilingi elfu themanini .
Naye
Meneja wa Kanda ya Iringa/Mbeya Jacob Omollo alikiri kuwepo kwa madai
hayo ya walinzi ya kutolipwa mishahara na kusema kuwa amewasiliana na
uongozi kutoka Dar es salaam ambapo alisema wamemtuma mtu kuja kuwalipa.
Alisema
kuwa kampuni imeshaanza kulipa mshahara wa mwezi saba na jumatatu
watamalizia kulipa mwezi wa nane ambapo walinzi hao walilipwa shilingi
80,000/- badala shilingi laki moja na ishirini (120,000/-).
Kuhusu
mkataba, meneja huyo alisema kuwa hajaingia mikataba yoyote na walinzi
hao isipokuwa kwa makubaliano fulani ambayo sio kwa maandishi.
Alisema kuwa walinzi hawajalipwa mishahara ya miezi miwili tangu tarehe 04.07.2014.
Kwa
Upande wake Katibu Mkuu wa TUPSE, Edison Kivelege aliongeza kuwa Iringa
ina jumla ya makampuni ya ulinzi binafsi 36 nyingi zikitoka nje ya mkoa,
lakini pamoja na hayo kampuni zenye ofisi azizidi kumi (10) na
kusababisha kukosa mawasiliano.
Alisema
kuwa chama kinapotaka kuwasiliana na wanachama wake kinapata shida ya
kuonana na viongozi kwa ajili yakutatua kero za wanachama kwa sababu
ofisi nyingi za waajiri zipo Mbeya, Morogoro na Dar es Salaam.
Alisema
kuwa kampuni nyingi hapa Iringa zinafanyakazi za udalali kwa sababu hiyo
kampuni hizo zinakuwa zinawaajiri walinzi wasiokidhi vigezo ambao
wanakuwa na uweledi mdogo kuhusiana na masuala ya ulinzi.
Katibu
Mkuu wa TUPSE huyo aliwaasa walinzi kuacha tabia ya kuhamahama makampuni
kwa sababu wanaji sababishia kupoteza mafao na uaminifu na kuwahimiza
wajisajili na chama hicho ili washiriki katika mabaraza ya majadiliano
na waajiri.
No comments:
Post a Comment