Meza
kuu, viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbarali na Kata ya
Chimala katika sherehe za kumtambulisha Kamanda wa Vijana (UVCCM) kwenye
matawi ya chama hicho.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM, Leonard Kitalima akizungumza jambo kabla
ya kumtambulisha Kamanda wa Vijana wa Kata ya Chimala.
Kamanda wa vijana wa UVCCM Kata ya Chimala, Francis Mtega akifuatilia kwa makini sherehe za kumtambulisha kwenye matawi.
Kamanda
wa vijana wa UVCCM Kata ya Chimala, Francis Mtega akifungua jiwe la
wakereketwa la UWT katika kilabu cha Songambele tawi la Mengele kwenye
sherehe za kumtambulisha kwenye matawi.
Kamanda
wa vijana wa UVCCM Kata ya Chimala, Francis Mtega akipandisha bendera
katika kijiwe cha wakereketwa cha Songambele tawi la Mengele kwenye
sherehe za kumtambulisha kwenye matawi.
baadhi ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa kwenye sherehe za kumtambulisha Kamanda wa Vijana kata ya Chimala
WANANCHI
nchini wametakiwa kutii amri halali zinazotolewa na jeshi la Polisi ili
kuepuka kujiingiza kwenye vurugu zisizokuwa na msingi wowote ikiwa ni
pamoja na kutii utawala wa sheria bila shuruti.
Wito
huo ulitolewa jana na Kamanda wa Umoja wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM),
Kata ya Chimala wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya,Francis Mtega, wakati
akitambulishwa kwenye matawi ya chama hicho.
Alisema
kazi ya Wanasiasa ni kuwaelekeza wananchi namna ya kufanya kazi ili
kupata maendeleo ili kuinua uchumi wao na sio kuwahamasisha kufanya
maandamano na kukaidi amri halali za jeshi la polisi hali inayozua
vurugu kwenye jamii na kurudisha maendeleo nyuma.
Aliongeza
kuwa endapo kila mtu atakuwa akijishughulisha na kazi za maendeleo
hakuna mwanasiasa atakayeweza kumshawishi kufanya maandamano wakati
akijua atapoteza kipato kutoka kwenye biashara yake anayoifanya.
Alitolea
mfano kwa umoja wa vijana kwamba ni taasisi kama zingine hivyo
zinapaswa kujiunga kwenye vikundi na kubuni vitega uchumi mbali mbali
ili kuweza kupata fedha kutoka kwenye Halmashauri ambazo hutenga
asilimia 5 ya mapato kila mwaka kwa ajili ya kusaidia vijana.\
Mtega
aliwaambia wananchi waliofurika katika mikutano ya utambulisho kuwa
moja ya majukumu yake ni kuhakikisha Chama kinashinda katika chaguzi
zake na kutoa wito kwa wananchi na wanachama kumuunga mkono ili kuwa na
nguvu ya pamoja.
Katika
utambulisho huo, Kamanda Mtega pia alizindua jiwe la wakereketwa wa
Umoja wa Wanawake(UWT) eneo la Songambele na kusimika bendera katika
Tawi la Mengele, Kilabu A na Kilabu B pamoja na tawi la Muala yote ya
Kata ya Chimala.
Mbali
na kufungua matawi hayo pia Kamanda huyo alioyeongozana na Madiwani wa
Kata, Viti maalumu na Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa CCM wilaya ya
Mbarali, Leonard Kitalima, walikabidhi kadi kwa wanachama wapya 170.
Sambamba
na shughuli hiyo pia viongozi hao walishiriki harambee ya ujenzi wa
choo katika Kilabu kinachoendeshwa na Umoja wa Wanawake tawi la Mengele
kinachogharimu zaidi ya shilingi Milioni 1.8.
Aidha katika harambee hiyo jumla ya shilingi 570,000 zilipatikana, ahadi shilingi 650,000 na kufanya jumla ya fedha zilizopatika kuwa Milioni 1.2 huku nguvu ikithaminiwa kufikia shilingi laki 5.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment