MNEC MAHAMUDU MADENGE |
Akiimba pamoja na waumini wa kanisa hilo |
Akipongezwa kwa nasaha nzuri |
Pongezei ziliendelea |
Akipewa zawadi ya CD moja baada ya kuzindua albamu ya mwimbaji huyo |
Baadhi ya waumini waliokuwepo |
wengine walikaa upande huu |
Hapa akiagwa kwa shamrashamra kubwa |
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha
Mapinduzi (NEC-CCM), Mahamudu Madenge amewaambiwa wakristo wenye nia ya
kushiriki maandamano yanayoitishwa na wanasiasa kwa nia mbaya kwamba yanawaweka
jirani na dhambi.
Hivi karibuni Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) kupitia Mwenyekiti wake Freeman Mbowe kilitangaza kuitisha
maandamano yasio na ukomo nchini nzima kwa lengo la kushinikiza kusitishwa kwa
Bunge la Katiba.
Wakati baadhi ya wanasiasa na wafuasi wa
chama hicho wakiyaunga mkono maandamano hayo ambayo hata hivyo yamedhibitiwa na
Polisi, wananchi wengi wamenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari wakiyaponda
kwa kile walichosema yanalenga kuvuruga amani ya nchi na kuchochea uhalifu.
“Tuache kufuata mikumbo ya siasa, kama
tunataka maandamano, tuandamane kuelekea makanisani na kufanya kazi inayompendeza
Mungu, tuishi kama alivyoishi Yesu” alisema Madenge anayeshikilia nafasi hiyo
nyeti kupitia manispaa ya Iringa.
Aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa albamu
ya injili ya muimbaji Yusuph Ngaluoka wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG)
la mjini Iringa, uliofanyika jana katika ukumbi wa Highlands mjini hapa.
Akiunga mkono kazi inayofanywa na
muimbaji huyo, Madenge alitoa mchango wa Sh Milioni moja na kuwataka watanzania
wengine kuunga mkono kazi za wasanii wa injili kama wanavyofanya kwa wasanii
wengine.
“Wasanii wa injili wanahubiri upendo,
amani na utulivu. Na sisi wote tunataka kuishi katika hali ya upendo, amani na
utulivu; ni muhimu tukawaogopa wanaotoka kutuingiza kwenye machafuko,” alisema
huku akishangiliwa na mamia ya waumini wa dini hiyo waliojitokeza katika
uzinduzi huo.
Alisema kama ilivyoandikwa katika kitabu
kitakatifu cha Biblia kwamba wenye moyo safi ndio watakaomuona Mungu ni muhimu
wanadamu wakatafakari na kuzipuuza kauli za wanasiasa zinazoweza kuwaondoa
katika sifa hiyo.
Wakati akichangia kiasi hicho cha fedha,
Madenge aliimba pamoja na waumini hao wimbo maarufu unaotumiwa na wakristo
kwenye shughuli mbalimbali wa “Mungu ni Pendo, apenda watu, Mungu ni Pendo
anipenda.”
Wakati wimbo huo ukiendelea kuimbwa,
Madenge alisema alichagua kufanya kazi ya jamii hivyo haoni sababu ya kuogopa
kushirikiana na watu wa makundi mbalimbali pale anapohitajika au kuombwa
kufanya hivyo.
Akishukuru kwa mchango wa Madenge na
nasaha zake, muimbaji huyo alimtaja kiongozi huyo kama mmoja wa viongozi wa
mfano mwenye moyo wa kusaidia jamii kila anapoombwa kufanya hivyo.
“Mungu akubariki ; nitalia kwa Mungu ili
akupe zaidi na zaidi na afanye kitu juu yako utakachokikumbuka katika maisha
yako yote,” alisema mbele ya mamia ya waumini wa kanisa hilo waliofurika katika
ukumbi huo.
No comments:
Post a Comment