Tuesday, September 23, 2014
BAADHI YA WAZAZI NA WALEZI WADAIWA KUTOROSHA WATOTO WASIFANYE VIZURI MITIHANI YA DARASA LA SABA,MMOJA ASHINDWA KUFANYA MTIHANI HUO BAADA YA KUTOROSHWA NA WAZAZI WAKE
HAWA NI WANAFUNZI WA DARASA LA SABA WANAOAGWA
WANAFUNZI NA WAZAZI WA KIWA KWENYE SHEREHE HIYO YA KUWAAGA WANAFUNZI WA DARASA LA SABA
VIONGOZI MBALIMBALI AKIWEMO DIWANI WA KATA YA NJOMBE MJINI AGREY MTAMBO ALIYECHAGULIWA KUPITIA CHADEMA PAMOJA NA MGENI RASMI MENEJA UENDESHAJI WA BENKI YA NJOCOBA
WALIMU WAKIELEKEA KUKABIDHI ZAWADI KWA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI
MENEJA UENDESHAJI WA BENKI YA WANANCHI WA NJOMBE NJOCOBA ALEX CHIZALEMA AKIWA KWENYE MAHAFARI YA DARASA LA SABA KATIKA SHULE YA MSINGI LUHUJI MJINI NJOMBE
Serikali Mkoani Njombe imeombwa kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya wazazi Waliotorosha na kuwashawishi watoto wao wasifanye vizuri mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi kwa sababu zao binafsi.
Rai hiyo imetolewa na meneja Uendeshaji wa Benki ya wananchi Njombe NJOCOBA bwana Alex chizalema Akiwa Mgeni rasmi kwenye mahafari ya kuwaaga wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Luhuji.
Bwana chizalema amesema kuwa wazazi wanatakiwa kutambua umuhimu wa kuwasomesha watoto wao kwaajili ya manufaa yao kwani wasipo soma taifa litaendelea kuwa na ongezeko la watoto wa mitaani na vijana wasiokuwa na ubunifu wa kufanya kazi kwa kukosa elimu.
Akizungumza kwa niaba ya Afisa elimu wa halmashauri ya Mji wa Njombe,Afisa elimu Ufundi wa halmashauri hiyo bwana Said Ibwe amesema amesikitishwa kupewa taarifa ya baadhi ya wazazi ambao wamehusika kutorosha watoto wao wasifanye mtihani wa darasa la saba mwaka huu.
Bwana Ibwe Amemuagiza mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Luhuji kutopeleka cheti cha mtoto huyo Nakwamba halmashauri kupitia idara ya Elimu itawafuatilia wazazi waliohusika kutorosha watoto wasifanye mitihani pamoja na kuwafundisha wafanye vibaya katika halmashauri hiyo.
Awali akitoa taarifa fupi ya shule Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Luhuji bi.Grace Mrwillo Amesema kuwa kati ya wanafunzi 87 waliotakiwa kufanya mtihani, mwanafunzi mmoja James Thomas Mlelwa ameshindwa kufanya mtihani huo baada ya wazazi wake kumtorosha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Norasco Kilasi akiwa na mwenyekiti wa mtaa wa Kwivaha Nathanael Maxona wakatoa wosia kwa wazazi na watoto wanaoagwa na wanaobaki
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment