Tuesday, September 23, 2014
DIWANI WA KATA YA IKUNA VALENTINO HONGORI AWATAKA VIONGOZI WA VIJIJI KUHAMASISHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA VIJIJI
HAWA NI WAJUMBE WA KAMAKA KATA YA IKUNA WAKIWA KWENYE UKUMBI WA KATA HIYO
DIWANI WA KATA YA IKUNA VALENTINO HONGORI AKIWA AMEKAA AKISIKILIZA TAARIFA INAYOWASILISHWA NA AFISA MTENDAJI WA KATA HIYO BWANA JOBU LUPONELO FUTE
Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Ikuna bwana Valentino Hongori amewataka watendaji na wenyeviti wa vijiji vya kata hiyo kutekeleza miradi kwa vitendo kwa kuwashirikisha wananchi ili kuharakisha maendeleo ya kata hiyo.
Akizungumza kwenye Kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata KAMAKA Bwana Hongori amewaagiza watendaji wa vijiji kuwasomea wananchi taarifa ya hesabu za mapato na Matumizi ili kuepukana na malalamiko toka kwa wananchi wanaowaongoza.
Aidha bwana Hongori amesema kuwa Michango mbalimbali kwaajili ya ujenzi wa maabara tatu inatakiwa kuendelea kwa kasi kama alivyoagiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa kila kata ihakikishe inajenga maabara tatu kwaajili ya masomo ya sayansi.
Amesema kuwa wenyeviti wa vitongoji wanatakiwa kuendelea na kazi ya uchangishaji na utekelezaji wa miradi iliyopo kwenye vijiji ikiwemo kutengeneza madawati katika shule za msingi na kwamba ni kijiji kimoja pekee cha Ikuna ambacho kimekwisha tekeleza zoezi hilo kwa kutengeneza madawati 50.
Afisa Mtendaji wa kata ya Ikuna bwana Jobu Luponelo Fute amesema wananchi na viongozi wa vijiji vya kata hiyo wanatakiwa kuonesha ushirikiano mkubwa kwa Mkuu wa shule ya sekondari Ikuna bi.Voronica Mfugale Ambaye amehamia hivi karibuni baada ya mkuu wa shule aliyekuwepo kustaafu katika kutekeleza miradi na majukumu ya shule.
Kwa upande wao wenyeviti wa vijiji wakitoa taarifa za utekelezaji wa miradi katika maeneo yao wamesema tayari wameanza ujenzi mbalimbali wa vyoo, madarasa na nyumba za walimu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment