Balozi
wa Tanzania Nchini Malawi, Patrick Tsere, mwenye suti katikati akipokea
picha ya ya wachezaji wa Mbeya City toka kwa wanahabari wa mkoa wa
Mbeya
TIMU ya mpira wa miguu ya Mbeya City
inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya imetakiwa kupeleka mwaliko wa
kuomba Timu za kujipima nguvu kutoka nchini Malawi ili kuimarisha ujirani
mwema kupitia sekta ya michezo.
Hayo yalibainishwa na Balozi wa Tanzania
Nchini Malawi, Patrick Tsere, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari wa
Mkoa wa Mbeya waliofanya ziara ya kimafunzo nchini Malawi na kumkabidhi picha
ya Wachezaji wa Mbeya City kwa lengo la kuitangaza timu hiyo kimataifa.
Balozi Tsere alisema atalichukua jukumu
la kuitangaza Mbeya City kama moja ya kazi yake nchini Malawi isipokuwa suala
muhimu ni uongozi wa timu hiyo kutuma barua za maombi ya kuzialika timu kutoka
Malawi ili kucheza michezo ya kirafiki hali ambayo itachangia kuimarisha
ujirani mwema na ushirikiano uliopo.
Suala na kuinadi Mbeya City limetokana
na maombi ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa waandishi wa
Habari waliofika Ofisini kwake kumuaga katika safari ya kuelekea nchini Malawi
ambapo alisema hivi sasa Mbeya city inajulikana kila kona nchini hivyo inabidi
itangazwe kimataifa.
Hata hivyo Waandishi hao wakiwa nchini
Malawi, mbali na kumkabidhi picha Balozi pia walipata kuzungumza na Waziri wa
Habari, Utalii na utamaduni wa Malawi, Kondwani Nankhumwa, ambaye alipogusiwa
kuhusiana na Mbeya city alisema haina tatizo atalifikisha kwa Afisa anayehusika
na michezo.
Alisema mbali na kulifikisha suala hilo
kwa afisa anayehusika pia alisema ni jukumu la Mbeya City kupeleka barua ya
mwaliko kwani kuna timu nyingi ambazo zinaweza kupambana na Mbeya city katika
michezo ya kirafiki.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment