Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, September 12, 2014

WASOMI WA NJOMBE KUTOKA VYUO VIKUU WAKUTANA KUJADIRI TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA NA KUSHUKA KWA MAADILI NJOMBE



 WASHIRIKI WA KONGAMAONO HILO


 DIWANI WA KATA YA NJOMBE MJINI [CHADEMA] AGRY MTAMBO AKICHANGIA HOJA



 MCHUNGAJI WA KANISA LA KILUTHEL DIOSISI YA KUSINI NJOMBE CHARLES MWANTEPELE AKITOA MADA


Vijana na wasomi wa kutoka vyuo mbalimbali Mkoani Njombe wametakiwa kubuni mbinu za  miradi ya Ujasiliamali  ikiwemo kilimo na ufugaji  wanapo  hitimu elimu  za vyuo vikuu  kwa kujikita katika sekta hiyo na kuajiri vijana wengine  katika Miradi yao ili kutatua tatizo la ajira kwa vijana.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa afya bwa Mkoa wa Njombe Mathias Gambishi  wakati akiwa mgeni rasmi katika Kongamano la wasomi wa Njombe la Njombe Intellectual  Association Lililowakutanisha wasomi wa kutoka halmashauri zote za mkoa wa Njombe kwa lengo la kujadili namna ya kutatua tatizo la ajira kwa vijana na kushuka kwa maadili.

Aidha bwana Gambishi amesema kuwa mmomonyoko wa maadili kwa vijana huenda ikawa ni sababu ya kukosekana kwa ajira  miongoni mwa vijana  na kuwataka wasomi wa mkoa wa Njombe kuonesha tofauti kwa kuanzisha miradi yao binafsi pasipo kutegemea kupata ajira selikalini.

Mchungaji wa kanisa la Kiluthel Tanzania Diosisi ya Kusini Njombe ambaye alikuwa mtoa mada Charles Mwantepele  amewataka vijana wanaotoka vyuoni wamekuwa ni chanzo cha kuharibu utamaduni katika jamii kwa kuvaa mavazi yasiyostahili kwa jamii,wazazi nao wamekuwa ni chanzo cha kuharibu malezi kwa watoto kutokana na kushindwa kukemea matendo hayo kwa watoto wao.

Aidha Mchungaji Mwantepele amesema suala la utandawazi limechangia kwa kiasi kikubwa kwa vijana kuharibikiwa kwani wamekuwa wakiangalia picha za x kwenye mitandao huku akisema vyombo vya habari navyo vimechangia kwa kurusha nyimbo zenye matusi na picha zenye mavazi ya kubana na uchi.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa  wafanyabiashara,viwanda  na kilimo mkoa wa Njombe bwana Oraph Mhema  amesema sekta ya Umma imekuwa kikwazo kikubwa kwa sekta binafsi  kutokana na kupangia kodi kubwa ya kukatisha tamaa na serikali kushindwa kuboresha baadhi ya Idara ikiwemo za utoaji wa leseni na huduma nyingine ambazo wakazi wa Njombe wakihitaji mpaka wafuate Mkoani Iringa na Mbeya.

Wakichangia mada zilizokuwa zikijadiliwa za Nini kifanyike kutatua tatizo la ajira na kushuka kwa maadili kwa vijana  baadhi ya wasomi waliohudhulia Kongamano hilo wamesema  ni vyema vijana wote wakaingia kwenye sekta binafsi na siyo kutegemea ajira serikalini huku wakiitaka serikali kuepukana na upendeleo wakati wa utoaji wa ajira.

Awali akifungua Kongamano hilo Mwenyekiti wa Njombe Intellectual Association Mkoa wa Njombe NIA Mwenyekiti wa Umoja huo bwana Pangani Msigwa amesema lengo la kuanzisha umoja huo ni kutaka kuibadilisha jamii ya Mkoa wa Njombe kuwa na mtazamo wa kujitegemea kiuchumi na yenye kutunza maadili kwa vijana wao.

Diwani wa kata ya Njombe mjini Agry Mtambo amewaomba wasomi hao kuwashirikisha na wasomi wa zamani katika kujadili mijadala mbalimbali wakiwemo walioko maofisini ili nao washuhudiye hoja zinazojadiliwa na wanavyoweza kukabiliana na malalamiko ya vijana dhidi ya sekta za umma.

No comments:

Post a Comment