Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, September 13, 2014

BARAZA LA BIASHARA MKOA WA NJOMBE LA KUTANA KUUNDA VIKUNDI KAZI

 MTAALAMU WA UBORESHAJI WA WA MAZINGIRA YA KUFANYA BIASHARA NA UWEKEZAJI  TOKA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA TNBC TANZANIA  NATIONAL BUSSNESS COUNCIL BWANA WILLY G.MAGEHEMA AKITOA SEMINA KATIKA UKUMBI WA AGREEMENT NJOMBE








 HAWA NI WATAALAMU NA VIONGOZI WA KUTOKA HALMASHAURI ZOTE ZA MKOA WA NJOMBE WAKIWEMO WAKURUGENZI NA WAKUU WA WILAYA
 MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI WA UPANDE WA KUSHOTO NA WA UPANDE WA NKULIA NI MWENYEKITI WA WAFANYABIASHARA ,VIWANDA NA KILIMO ORAPH MHEMA MKOA WA NJOMBE

 KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI SARAH DUMBA,WA PILI KUTOKA KUSHOTO NI KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE JACKSON SAITABAHU NA WA TATU KUTOKA KUSHOTO NI MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI NA WA NNE KUTOKA KUSHOTO NI MWENYEKITI WA WAFANYABIASHARA MKOA WA NJOMBE ORAPH MHEMA NA WA MWISHO NI MUWAKILISHI KUTOKA TNBC









ERNEST MKONGO AKIWASILISHA AKIZUNGUMZA NAYE HABARI ITAKUJIA HIVI PUNDE.....
Na Michael Ngilangwa

 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Keptain Mstaafu Aseri Msangi amezindua baraza la Biashara la Mkoa wa Njombe  litakalo boresha mazingira ya biashara na Uwekezaji  na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara Ili kuboresha uchumi wa Mkoa na mwananchi Binafsi.

Akizungumza  Wakati wa Uzinduzi wa baraza la Biashara lililofanyika Mkoani Njombe Mkuu wa Mkoa Keptain Mstaafu Aseri Msangi amesema wafanyabiashara na wawekezaji wanatakiwa kuwekeza katika Mkoa wa Njombe kwa kujenga Viwanda mbalimbali vikiwemo vya kusindika unga na Matunda ili kusaidia kuongeza ajira kwa vijana.

Katika Uzinduzi wa baraza hilo wamefanikiwa kuunda Vikundi kazi  vyenye kamati sita  vitakavyosimamia ufanikishaji wa kuboresha mazingira ya biashara na Uwekezaji Ikiwemo Viwanda na Biashara,Ardhi na Maliasili,Nishati na Madini,Mifugo na Uvuvi,Viwanda na Biashara ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi Mkoani Njombe.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa baraza hilo Mtaalamu wa Uboreshaji mazingira ya kufanya biashara na Uwekezaji kutoka Baraza la Taifa la Biashara TNB Bwana  Willy Magehema  amesema  lengo kuu la uzinduzi wa Baraza hilo   Ni kuboresha mazingira ya  biashara na uwekezaji kwa kutatua kero,kuibua fursa na kuzinadi ili kuhakikisha uchumi wa mkoa na Mtu mmoja mmoja unaongezeka.

Aidha Bwana Magehema amesema  Baraza hilo ni mshauri mkuu wa Mkuu wa Mkoa na kwamba sekta binafsi ndiyo muhimili wa uchumi wa Nchi Ambapo kero zikitatuliwa wafanyabiashara mbalimbali wataendesha shughuli zao pasipo kuwepo kwa changamoto nyingi zitakazo kwamisha na kwamba kamati zilizoundwa zitasaidia kutatua matatizo yanayowakabili wafanyabiashara na sekta binafsi.


Kwa upande wake mwenyekiti wa wadfanyabiashara,Viwanda na Kilimo mkoa wa Njombe Oraph Magehema amesema kuwa kuundwa kwa baraza hilo kutamunufaisha  mfanyabiashara  kwani baraza hilo litatatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

No comments:

Post a Comment