Friday, September 12, 2014
KAMPUNI YA MARIET NATURAL FOODS COMPANY LTD YATARAJIA KUAJIRI WAFANYAKAZI 30 KATIKA KIWANDA CHA KUSINDIKA JUICE ZA MATUNDA NA CHIRI SORCE MJINI NJOMBE
KAZI NA MAZUNGUMZO YA SIMU VINAKWENDAA? HUYU NI MFANYAKAZI YUPO KAZINI HAPA
HIZI NI JUICE ZA MATUNDA YA ASILI YNAYOPATIKANA PORINI MAARUFU KWA JINA LA MISASATI
HAYA NI MAZAO YANAYOZARISHWA NA KIWANDA HICHO
HII NI MITAMBO YA KUTENGENEZEA JUICE IKIWA INATARAJIWA MINGINE MIKUBWA KUFIKISHWA SIKU ZA HIVI KARIBUNI
HAWA NIN WAFANYAKAZI WA KIWANDA HICHO CHA KUSINDIKA VYAKULA MBALIMBALI IKIWEMO JUICE ZA MATUNDA NA SOSEJI
HUYU NI MKURUGENZI WA MARIET NATURAL FOODS BI.MARIETA PUTIKA AKIWA OFISINI KWAKE
HUYU NI MENEJA MASOKO WA KAMPUNI HIYO
Na Michael Ngilangwa
Wananchi Mkoani Njombe wameshauriwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa ya matunda mbalimbali yakiwemo ya asili na yasiyo ya asili na kupeleka katika viwanda vinavyofanya kazi ya kusindika Juice za Matunda ya asili ili kuinua uchumi wa kila mmoja.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Mariet Natural Food Kamapan Limited bi.Marieta Putika wakati akizungumza na Uplands fm akiwa Ofisini kwake na kusema kuwa shirika hilo linajihusisha na usindikaji wa juice za matunda ya asili tangu mwaka 2001.
Aidha Bi Putika amesema kuwa jamii inatakiwa kutumia vyakula vya asili ikiwemo matunza yasiyochanganywa na kemikali mbalimbali ambayo yamekuwa yakihimizwa na wataalamu.
Bi.Putika amesema kuwa Kampuni hiyo ya kusindika Juice za Matunda imefanikiwa kuzalisha juice kwa kiasi kikubwa baada ya kupata msaada kutoka shilika la MUVI ambalo limewaunganisha wakulima wa zao la nyanya na kampuni hiyo na kuongeza uzarishaji kutoka nusu ya tani zilizokuwa zikizarishwa hapo awali na kufikia tani mbili kwa siku.
Amesema kuwa kampuni hiyo ya kusindika juice za matunda imekuwa ikitumia mazao mbalimbali ya vyakula yakiwemo nyanya,matunda ya asili,nanasi pamoja na kutengeneza chiri sosi Ambapo soko la mazao yanayozalishwa yamekuwa yakipatikana Njombe na mikoa mingine ya jirani.
Bi.Putika Ameshukuru shirika la Muunganisho wa wajasiliamali vijijini MUVI Kwa kuwaunganisha na Kampuni hiyo kwani wakizalisha zao la nyanya soko lao kubwa ni kwa kampuni hiyo jambo ambalo limetoa fursa ya kujiajiri na kuajiliwa kwa baadhi ya vijana katika kampuni hiyo na kwenye kilimo cha nyanya.
Kampuni hiyo kwa sasa inamatarajio ya kupeleka mitambo mingine ya kisasa ambayo itasaidia kuzarisha tani sita kwa siku na kuongeza watumishi kutoka idadi ya wafanyakazi watano na kufikia 30 jambo ambalo litasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana mjini Njombe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment