Thursday, September 25, 2014
NMB NJOMBE YAKABIDHI MADAWATI 200 KWA MKUU WA MKOA WA NJOMBE
MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI AKITOA HOTUBA YAKE BAADA YA KUKABIDHIWA MADAWATI HAYO
Benki ya NMB Tawi la Njombe Jana Imekabidhi Jumla ya Madawati 200 Kwa ajili ya Kusaidia Kupunguza Tatizo la Madawati Katika Shule za Msingi Mkoani Njombe Kama Moja ya Sera ya Benki Hiyo Kushiriki Katika Shughuli za Kijamii.
Akikabidhi Madawati Hayo Kwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Asseri Msangi,Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Njombe Bwana Hemed Risasi Amesema Kuwa Hatua Hiyo Imekuja Kufuatia Uhitaji wa Madawati Katika Shule Mbalimbali Mkoani Njombe.
Bwana Risasi Amesema Kuwa Ugawaji wa Madawati Hayo ni Muendelezo wa Benki Hiyo Kutoa Misaada Mbalimbali Katika Sekta ya Elimu na Afya Ambapo Kwa Mwaka Huu Benki Hiyo Imetenga Shilingi M Bilioni Moja Kwa ajili ya Sekta Hizo.
Akizungumza Mara Baada ya Kupokea Madawati Hayo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captein Mstaafu Asseri Msangi Ametumia Fursa Hiyo Kupongeza Jitihada za Benki Hiyo Huku Akiwataka Wadau Mbalimbali Kuiga Mfano wa Benki Hiyo.
Msangi Amesema Kuwa Licha ya Kwamba Hakuna Wanafunzi Wanaokaa Chini Katika Shule za Mkoa wa Njombe Lakini Bado Wanafunzi Hao Wamekuwa Wakikaa Kwa Kubanana Jambo Ambalo Wazazi na Jamii Nzima Inapaswa Kuendelea Kuchangia.
Katika Hatua Nyingine Amesema Kuwa Madawati Hayo Yatasambazwa Katika Halmashauri Zote za Mkoa wa Njombe Ambapo Itasaidia Katika Kupunguza Adha Hiyo Katika Sekta ya Elimu.
Septemba 24 Mwaka Huu Benki ya NMB Tawi la Njombe Imegawa Madawati 1oo Katika Halmashauri ya Wilaya Njombe Yenye Thamani ya Shilingi Milioni Tano na Kusaidia Kupunguza Tatizo Kubwa la Madawati Lililokuwa Linaikumba Halmashauri Hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment