HAPA NI NJE YA UWANJA WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHEL TANZANIA MELINZA KWENYE MITI KANDO YA BARABARA KUU YA NJOMBE SONGEA
HAWA NI WANANCHI WA MTAA WA MELINZE WAKISHUHUDIA TUKIO LA KUFARIKI KWA MAREHEMU HUYO BWANA Evaristo Mgeni
MKAZI WA MTAA WA MELINZE AKIWA ENEO ALILOLALA USIKU WOTE HADI ALIPOKUJA KUTAMBULIWA NA WANANCHI
ASKALI POLISI WAKIUCHUKUWA MWILI WA MAREHEMU TAYARI KWA KUUPELEKA HOSPITALI YA KIBENA
Na Michael Ngilangwa -Njombe
Mtu Mmoja mkazi wa mtaa wa Melinze Evarist Mgeni amekutwa akiwa amefariki dunia
katika uzio wa mlango wa Kuingia kanisa la Kiinjili la Kiluthel Tanzainia Usharika wa
Melinze mapema leo Huku chanzo cha Tukio hilo kikishindwa kufahamika mara moja.
Wakizungumza na Uplands fm Baadhi ya mashuhuda wa Tukio hilo wamesema wameweza
kumuona marehemu Evarist Akiwa amelazwa kifudifudi kwenye miti ya Hekya ya kanisa
la Kiinjili la Kiluthel Tanzania la Melinze Ambapo wamepeleka taarifa kwa viongozi wa
mtaa ndipo nao wakapeleka taarifa hizo kwa jeshi la polisi na kuimarisha usalama.
Wamesema kuwa tukio hilo huenda likahusishwa na mauaji Nakwamba taarifa kamilii
kama ameuwawa ama amefariki mwenyewe zitathibitishwa na Mganga Mkuu wa Hospitali
ya Kibena ambako Mwili wa Marehemu huyo umepelekwa kwa uchunguzi zaidi Ambapo
wameomba serikali za mitaa ziendelee kuimarisha ulinzi shirikishi ili kutokomeza matukio
kama hayo.
Akizungumza akiwa eneo la Tukio Afisa Mtendaji wa Kata ya Mjimwema bwana Gehazi
Mkongwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba chanzo cha Tukio hilo bado
kinaendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Ambapo tukio limetokea
majira ya saa isiyofahamika ya usiku wa kuamukia leo.
Aidha bwana Mkongwa amewaomba wananchi kuonesha ushirikiano kwa viongozi wao
katika kutoa taarifa za matukio yanapokuwa yamejitokeza katika maeneo yao Kwani
kumekuwa na baadhi ya wananchi hushindwa kutoa taarifa kwa wakati kwa viongozi
matukio ya mauaji yanapokuwa yametokea.
Matukio ya Mauaji yamekuwa yakijitokeza kwa baadhi ya maeneo katika halmashauri za
Mkoa wa Njombe Huku wengine wakivamiwa,kujeruhiwa na kupolwa mali zao Ambapo
Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe limekuwa likihamasisha viongozi kwa kushirikiana na
viongozi wa mitaa kuunda ulinzi shirikishi lili kuzuaiya matukio kama hayo.
No comments:
Post a Comment