Thursday, September 25, 2014
MBUNGE MSTAAFU WA MUFINDI KASKAZINI JOSEPH MUNGAI AMEAHIDI KUCHANGIA MILIONI 20,MKUU WILAYA MUFINDI EVARISTA KALALU NAYE ATOA AHADI YA BATI 20 KWAAJILI YA KUKAMILISHA UJENZI WA KANISA LA KKKT MALANGALI
ASKOFU WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHEL TANZANIA DAYOSISI YA KUSINI JAPHET MENGELE AKIZUNGUMZA AKIWA KATIKA KANISA ALILOANZA KULIJENGA MAREHEMU THOMASI BANGU MALANGALI
WANANCHI MBALIMBALI WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA NENO LA MUNGU AMBALO LINATOLEWA NA MAASKOFU KATIKA KANISA HILO SIKU YA MSIBA WA MZEE BANGU
VIJANA MBALIMBALI AKIWEMO WILIARD MAIM,AGREY NYASI WAKIWA NA WENZAO KWENYE MSIBA HUO
NDUGU WA MAREHEMU AKIWEMO MKE WA MAREHEMU BANGU NA WATOTO WAKE
HILI NDILO KANISA AMBALO MAREHEMU ALIANZA KULIJENGA NA HAPA LIPO HATUA ZA MWISHO
HAPA SAFARI YA KUELEKEA MAKABURINI KUMZIKA MZEE BANGU
Mbunge Mstaafu Wa Mufindi Kaskazini Joseph Mungai Ameahadi Kuchangia Milioni 20 Huku Mkuu Wa Wilaya Ya Mufindi Mkoani Iringa Bi.Evarista Kalalu Akiahidi Kupeleka Bati 20 Kwaajili Ya Kukamilisha Ujenzi Wa Kanisa Ambalo Alianzisha Kulijenga Marehemu Mwalimu Mstaafu Tomasi Asangye Bangu Malangali.
Akizungumza Mbele Ya Maaskofu Mbalimbali Tanzania Wakiongozwa Na Askofu Wa Dayosisi Ya Kusini Japhet Mengele Ambao Wamefika Kuuzika Mwili Wa Marehemu Thomas Bangu, Mbunge Mstaafu Joseph Mungai Amesema Kwa Kutambua Jitihada Za Marehemu Huyo Za Kufundisha Na Kuendeleza Elimu Ya Ufundi Stadi Wakristo Na Wananchi Kata Ya Malangali Wanatakiwa Kuiga Mfano Wake.
Aidha Bwana Mungai Amesema Kuwa Marehemu Bangu Alianza Kujenga Kanisa La Kiinjili La Kiluthel Tanzania Katika kijiji cha Mwilavila Kata Ya Malangali Ili Kusaidia Kupunguza Umbari Mrefu Kwa Wakristo Wa Kata Hiyo Ambao Wamekuwa Wakisafiri Hadi Kijiji Jirani Cha Isimikinyi Kupata Huduma Za Kiroho.
Mkuu Wa Wilaya Ya Mufindi Mkoani Iringa Evarista Kalalu Amesema Serikali Inatambua Uwepo Wa Marehemu Mwalimu Mstaafu Thomas Bangu Ambapo Amesema Wananchi Na Wadau Mbalimbali Wa Huduma Za Kiroho Wanatakiwa Kuunga Mkono Jitihada Hizo Pamoja Na Wanafunzi Kuthamini Masomo Ya Ufundi Stadi Kwa Manufaa Yao.
Awali Akiwakaribisha Wageni Mbalimbali Katika Kanisa Ambalo Marehemu Mwalimu Thomas Bangu Alianza Kujenga Askofu Wa Kanisa La kiinjili la Kiluthel Tanzania Dayosisi Ya Kusini Japhet Mengele Akiwa Na Mkuu Wa Kanisa La Kiinjili La Kiluthel Tanzania Askofu Dkt Alex Malasusa Wamesema Wakristo Na Wadau Wa Dini Wanatakiwa Kuchangia Michango Mbalimbali Ili Kukamilisha Ujenzi Wa Kanisa Hilo Ambalo Lipo Katika Hatua Za Mwisho Kukamilika.
Samwel Thomas Bangu Na Washiriki Mbalimbali Akiwemo Mwalimu Judith Kisinini Wakatoa Historia Ya Marehemu Thomas Bagu Kwamba Alizaliwa June 29 Mwaka 1918 Akiwa Katika Kijiji Cha Mdandu Wilaya Ya Wanging'ombe mkoani Njombe Ambapo Alikuwa Mwalimu Wa Ufundi Stadi Katika Shule Ya Sekondari Malangali Wilayani Mufindi Mkoani Iringa Hadi Alipo Staafu Mwaka 1973.
Marehemu Thomas Asangye Bangu alifariki mnamo sept 20 na kuzikwa septemba 24,2014 katika makaburi yaliyopo kijiji cha Mwilavila kata ya Malangali Wilayani Mufindi na Kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali Nchini Tanzania wa serikali,Siasa na Kidini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment