Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, April 16, 2014

MKUU WA MKOA WA NJOMBE LEO AMEWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA MAJI UKALAWA



HILI NI TENKI LA MAJI AMBALO LINAENDELEA KUJENGWA KATIKA KIJIJI CHA UKALAWA KATA YA IKONDO WILAYANI NJOMBE

KUNDI LA NGOMA ZA ASILI KUTOKA KANIKELELE WAKIFANYA MAMBO HADHARANI KWA KUTOA BURUDANI SIKU YA UJIO WA MKUU WA MKOA WA NJOMBE



WANANCHI WA KIJIJI CHA UKALAWA WAKISIKILIZA KWA UMAKINI HOTUBA YA MKUU WA MKOA
KAIMU MHANDISI WA MAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE AKIKABIDHI TAARIFA FUPI KWA MKUU WA MKOA WA NJOMBE
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AKIMKARIBISHA MGENI RASMI AKIWA KIJIJI CHA UKALAWA LEO
 MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA AKITAMBULISHA UGENI KWA WANANCHI WA KIJIJI CHA UKALAWA
 MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN NMSTAAFU ASERI MSANGI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA IKONDO LEO




MKUU WA MKOA  WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI AKIWEKA JIWE LA MSINGI


NGOMA YA LIMUDOYA TOKA KANIKELELE LUPEMBE WAKIBURUDISHA  WAGENI WALIOFIKA KATIKA KIJIJI HICHO KUWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA TENKI LA MRADI WA MAJI UKALAWA





Mkuu wa mkoa wa Njombe Keptain Mstaafu Aseri Msangi  jana amehitimisha ziara yake ya siku tatu wilayani Njombe kwa kuweka jiwe la msingi katika tenki la mradi wa maji  unaotekelezwa kijiji cha Ukalawa ambao utagharimu zaidi ya shilingi milioni mia tano.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ukalawa mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye Tenki la mradi wa maji unaotekelezwa kijijini hapo Mkuu wa mkoa wa Njombe Keptain mstaafu Aseri Msangi amewataka wananchi kushiriki kikamilifu kuchangia ujenzi wa mradi huo huku viongozi wa vijiji na halmashauri kusimamia ukamilishaji wa miradi ambayo haijakamilika na iliyowekewa mawe ya misingi.

Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa huyo Keptain Msangi amemuagiza afisa taarafa kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji na kata kuhakikisha wanafunzi wote wa shule ya sekondari  Ukalawa wanahamia  katika hosteli za shule  hiyo huku wazazi wakitakiwa  kuchangia chakula shuleni ili kuwaondoa wanafunzi wasiishi katika nyumba za kupanga mitaani.

Akisoma taarifa fupi ya utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Ukalawa kaimu muhandis wa maji wa halmashauri ya wilaya ya Njombe bwana Joakimu Sanga amesema kuwa mradi huo utagharimu shilingi milioni mia tano themanini na mbili,na laki mbili na sitini na tisa elfu mia mbili sitini na moja.

Muhandisa huyo bwana Sanga amesema kuwa mradi huo unatarajia kukamilika  mnamo june 30 mwaka huu utahudumia watu elfu mbili mia nane na saba ambapo wananchi walitakiwa kuchangia asilimia mbili .tano ikiwa mpaka sasa wamechangia shilingi milioni tatu na laki moja.

Awali wakiuliza maswali wananchi wa kijiji cha Ukalawa wameiomba serikali kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo kutengeneza barabara,kufukuza wanyama waharibifu wa mazao,kubadilishiwa mbolea ya Yalamila na minjingu kwa madai mbolea hizo hazifai kwa kilimo cha chai.

No comments:

Post a Comment