Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, April 15, 2014

MKUU WA MKOA WA NJOMBE AAGIZA KUFUKUZWA KWA MWENYEKITI WA BODI YA SHULE YA SEKONDARI LUPEMBE


 WA UPANDE WA KULIA NI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE PAUL MALALA NA WA PILI KUTOKA KULIA NI KATIBU WA MKUU WA MKOA DANIEL NGALUPELA NA WA TATU KUTOKA KULIA NI MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE VALENCE KABELEGE WAKIWA KATIKA OFISI YA MKUU WA SHULE YA SEKONDARI LUPEMBE
 WAKUU WA IDARA WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE
 MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN  MSTAAFU ASERI MSANGI  AKIWA KATIKA OFISI YA MKUU WA SHULE YA SEKONDARI LUPEMBE AKIPATIWA TAARIFA YA MAENDELEO YA SHULE
 DIWANI WA KATA YA LUPEMBE BI.TWILUMBA WAPALILA AKIJIBIA BAADHI YA HOJA ZA KUSHIRIKI KATIKA  MAENDELEO YA SHULE HIYO
 MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE PAUL MALALA
 KAIMU AFISA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI
 MKURUGENZI PAUL  MALALA AKIWA NA MTUMISHI WAKE  KAIMU MKUU WA IDARA WAKIELEKEA KUKAGUA MAJENGO YANAYOJENGWA KATIKA SHULE YA SEKONDARI LUPEMBE WAKIUONGOZA UGENI HUO WA MKOA

 HAPA MKUU WA MKOA ANAELEKEA KUKAGUA MAJENGO AMBAYO NI NYUMBA YA MWALIMU,CHOO NA MAABARA YA SHULE
 HILI NI  JENGO LA MAABARA MPYA INAYOJENGWA  SHULE YA SEKONDARI LUPEMBE



 HILI NI JENGO LA NYUMBA YA MWALIMU LINALOJENGWA KATIKA SHULE HIYO

 MKUU WA MKOA WA NJOMBE AKITOKA KUKAGUA JENGO LA CHOO KIPYA KINACHOJENGWA SHULENI HAPO

 HAWA NI WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI LUPEMBE WAKIWA DARASANI
 HAWA NI WAKUU WA IDARA WAKIONGOZWA NA AFISA HABARI WILAYA LUKERO MSHAURA WAKIPEANA MAWAZO NA DR.CONRAD UGONILE KATIKA SHULE YA SEKONDARI LUPEMBE
MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU ASERI  MSANGI NA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH  DUMBA  WAKIWA KATIKA OFISI YA WALIMU SHULE YA SEKONDARI LUPEMBE

 WALIMU WAKIULIZA MASWALI NA KERO ZINAZOWAKABILI BSHULENI  HAPO

 MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA AKITOLEA UFAFANUZI JUU YA KUUZWA KWA MSITU HUO  WA SHULE
AFISA TAARAFA YA LUPEMBE BWANA BALTAZARY MVEYANGE AKIJIBU MASWALI YA PAPO KWA PAPO YALIOULIZWA NA MKUU WA MKOA WA NJOMBE

Mkuu wa mkoa wa Njombe keptain Mstaafu Aseri Msangi ameagiza kufukuzwa kwa mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Lupembe kufuatia kuwepo kwa malalamiko toka kwa walimu ya kutoshilikishwa katika maamuzi ya mali za shule hiyo ikiwemo kuuzwa kwa msitu wa miti ya shule pasipo kuwashirikisha.

Wakizungumza mbele ya mkuu wa Mkoa wa Njombe walimu wa shule ya sekondari Lupembe pamoja na kulalamikia kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazo ikabili shule hiyo za ukosefu wa miundombinu ya maji,uchakavu wa nyumba za walimu pamoja na kuwepo kwa makato ya mishahara ya walimu hao pia wamelalamikia kuishi katika mazingira magumu jambo lililosababisha wanafunzi kutokuwa na ufauru mzuri.

Aidha walimu hao Wamesema kuwa moja ya lengo la kuhamasika kupanda miti hiyo ilikuwa ni kuja kusogeza miundombinu ya maji na kujenga nyumba za walimu ambapo wameshangazwa kuona bodi ya shule imeingia na kuuza msitu huo pasipo wao kushirikishwa huku wakiendelea kuishi katika mazingira magumu kwa kufuata maji mtoni ambako wanatembea umbali wa takribani kilomita tatu jambo linalosababisha wanafunzi kukosa muda wa kujisomea.

Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi. Sarah Dumba akatolea ufafanuzi juu ya kuuzwa kwa msitu huo kwamba uliuzwa kwa shilingi milioni 80 na bodi ya shule hiyo kwa madai wanahitaji fedha za   kukarabati nyumba za walimu na kupeleka maji shuleni hapo  lakini ameshangazwa kusikia bado kuna tatizo la maji shuleni hapo huku bodi hiyo ilisema imekwisha kupeleka pamoja na kukurabatiwa kwa nyumba za walimu hao.

Aidha bi.Dumba amesema zoezi hilo lilifanyika tangu mwaka 2012 ambapo  alipata taarifa ya kukatwa kwa msitu wa miti ya shule hiyo na kumuuliza mkurugenzi aliyekuwepo wakati huo Mohamed Mkupete ambapo hakuna utekelezaji wake uliochukuliwa ambapo amesema alipoihoji bodi ya shule hiyo ilisema yenyewe ndiyo yenye mamlaka juu ya kila kitu kuhusiana na shule hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Keptain Mstaafu Aseri Msangi ameagiza kuondolewa kwa mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Lupembe ambapo halmashauri inatakiwa kupeleka wakaguzi na tume ya kupambana na kudhibiti Rushwa  TAKUKURU Ili kubaini mapungufu yaliofanyika na ikibainika kuna ubadhilifu wa mali za shule hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Ziara ya Mkuu wa mkoa wa Njombe jana ilikuwa katika kata ya Lupembe kwa kukagua maendeleo ya shule ya sekondari Lupembe na baadae nkuongea na wananchi ambapo alifanikiwa kukagua majengo ya maabara,nyumba ya mwalimu pamoja na choo chenye matundu nane ujenzi utakaogharimu shilingi milioni mia mbili sitini na saba hadi kukamilika kwake ambapo halmashauri imekwisha kupeleka shilingi milioni 13 katika ujenzi unaoendelea kwa sasa Na leo ziara hiyo inaendelea vijiji vya kata za Ikondo vya ukalawa mkoani Njombe.

No comments:

Post a Comment