Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, April 16, 2014

JUMUIYA YA KANISA LA KILUTHEL TAZANZANIA DIOSISI YA KUSINI YA LARWAY NJOMBE YAKABIDHI MSAADA KWA WAFUNGWA NJOMBE

 KAIMU AFISA MKAGUZI MSAIDIZI  WA GEREZAL LA NJOMBE GRACE SUMARI  AKIONGEA MARA BAADA YA KUFANYIKA TENDO LA KUKABIDHI MISAADA HIYO

 WANACHAMA WA JUMUIYA HIYO WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KAIMU MKUU WA GEREZA LA NJOMBE
 MWENYEKITI WA JUMUIYA YA KILUTHEL TANZANIA DIOSISI YA KUSINI YA LERWAY ADRIANO MSEMWA

 WA UPANDE WA KULIA NI KATIBU WA JUMUIYA HIYO MWINJILISTI AHABU NG'EVE,NA WA UPANDE WA KULIA NI MWENYEKITI WA JUMUIYA ADRIANO MSEMWA

Jumuiya ya kanisa la kiluthel Tanzania Diosisi ya Kusini ya Lerway jana imekabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali kwa wafungwa wa magereza ya Njombe yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja na sitini ambapo hatua hiyo ni muendelezo wa taasisi na mashirika kwenda kusaidia wafungwa na wagonjwa mbalimbali.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo mwenyekiti wa Jumuiya ya kiluthel diosisi ya kusini bwana Adriano Msemwa amesema kuwa jumuiya hiyo ina mipango mikakati ya kuendelea kuwasaidia na watu wengine ikiwemo kuwatembelea wagonjwa,yatima na wasiyojiweza ili kuwasaidia misaada hiyo.

Aidha bwana Msemwa amewataka wadau na taasisi mbalimbali mkoani Njombe kutambua umuhimu wa kuwasaidia watu wenye ulemavu,wagonjwa na wafungwa ambapo pamoja na mambo mengine amesema kuwa kutoa ni moyo hivyo kila mmoja anatakiwa kutoa misaada hiyo na kama njia mojawapo ya kutekeleza upendo katika kristo.

Grace Sumary ni Afisa Mkaguzi msaidizi Wa gereza mkoa wa Njombe ameshukuru kwa jitihada zinazofanywa na taasisi na mashirika mbalimbali ya kijamii ambayo yamekuwa yakifika katika gereza hilo na kuwasaidia wafungwa mahitaji mbalimbali ambapo amewataka Ndugu mbalimbali kufika kuwasaidia ndugu zao waliopo gerezaji hapo.

Katibu wa Jumuiya hiyo Mwinjilist Ahabu Ng'eve wananchi wanatakiwa kutambua kuwa wafungwa wanahitaji kupatiwa faraja ili wafungwa hao waweze kubadilika watakapo maliza kifungo chao na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi badala yake wafuate vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo wake.

No comments:

Post a Comment