MCHUNGAJI WA KANISA LA FREE PENTECOSTAL CHURCH OF TANZANIA LA TARAAFA YA MALANGALI LWINUSO LUTUMO AKIWA OFISINI KWAKE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
KATIKA SUALA LA NDOA NALO AMEONYA WATUMISHI MBALIMBALI WA KIDINI NA WASIYO WA KIDINI KUTOZISALITI NDOA ZAO NA KWAMBA WAKIWA SAFARINI WASAFIRI WOTE PALE INAPOBIDI
KWA MSISITIZO MCHUNGAJI LUTUMO AMESEMA SI VYEMA KUSALITI NDOA ZAO
KWA WANANDOA WALIOFUNGA PINGU ZA MAISHA MBELE YA VIONGOZI WA DINI
Mchungaji wa kanisa la Free PENTECOSTAL CHURCH OF TANZANIA FPCT la Malangali Wilayani Mufindi mkoani Iringa Lwinuso Lutumo amewataka viongozi wa dini kukemea vikali tabia ya baadhi ya waumini ambao wameendekeza kushusha maadili ya kidini na kijamii kwa kuingia katika nyumba za ibada wakiwa na mavazi yalio kinyume na maadili ya Kikanisa.
Akizungumza na mtandao huu leo Mchungaji Lutumo amesema kuwa viongozi wa dini wanatakiwa kuhamasisha waumini wa dini mbalimbali kuwatembelea wagonjwa na kutoa misaada mbalimbali ili kuwanusuru na kuwasaidia kujikwamua na hali ngumu walizo nazo kwani kumekuwa na baadhi ya wagonjwa hupoteza maisha yao kutokana na kukosa misaada.
"Soma Marko 16:15-18,Yohana 10:1-15,Yohana 21:21-23 ambayo yanahamasisha watumishi kuwatumikia waumini na jamii inayowazunguka kwa kuwasaidia" Ameyasema mchungaji Lwinuso Lutumo.
Aidha bwana Lutumo amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya watumikshi wa Mungu wamekuwa wakitegemea kusaidiwa na waumini wao jambo ambalo linaweza kuonesha kuwa huenda watumishi wanatoa huduma za kiroho kwa kutegemea maslahi hali inayosababisha maadili ya kidini kushuka Ezekiel 3:18-23,1 Timetheo 3:1-8,2 Timetheo 3:1-6.
Katika hatua nyingine mchungaji Lutumo ameishauri jamii pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo watumishi wa dini na serikali kutowaacha wanandoa wao pindi wanaposafiri ili kuepukana na vishawishi vinavyoweza kujitokeza na kwamba jambo hilo limekuwa likipelekea ndoa nyingi kuharibika na kuongezeka kwa mitala huku baadhi ya wananndoa hali ambayo inachangiwa na mmomonyoko wa maadili ya dini.
Kwa maoni na ushauri juu ya kusoma Biblia wasiliana nasi kupitia SIM NAMBA,0758351992 tunaombea kwa njia ya simu kwa wenye shida mbalimbali.
No comments:
Post a Comment