VIFAA VYA KUFULIA MADINI YA CHUMA NA MATENGENEZO YA MIUNDOMBINU YA BARABARA VYAANZA KUFIKA
Rais Jakaya Kikwete Amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Keptein Mstaafu Aseri Msangi Pamoja na Watendaji Wake Kufuatili Shilingi Bilioni Kumi Zilizotolewa na Serikali Kwa Ajili ya Kuwalipa Wakulima wa Mahindi Wilayani Ludewa Ambao Wanaidai Serikali.
Aidha Rais Kikwete Pia Imeitaka Halmashauri ya Makete Kwa Kushirikiana na Uongozi wa Mkoa wa Njombe Kuwabana Watu Wanaonunua Zao la Pareto Kutoka Kwa Wakulima Bila Kufuata Taratibu Zinazohusika na Kukwepa Kulipa Kodi na Kuwakandamiza Wakulima wa Zao Hilo.
Akiongea Wakati wa Majumuisho ya Ziara Yake ya Kikazi ya Takribani Siku Sita Mkoani Njombe Kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Rais Kikwete Ameruhususu Sekta Binafsi Kununua Mahindi ya Wakulima Yaliyosalia Kwa Wakulima.
Halikadhali Rais Kikwete Amewataka Viongozi wa Mkoa wa Njombe Kuendelea Kusisitiza Mazao ya Biashara Ikiwemo Miti ya Mbao ,Kahawa ,Matunda na Mbogamboga Pamoja na Kufufua Zao la Pareto
Akielezea Kuhusu Miundombinu Mbalimbali Mkoani Njombe Rais Kikwete Amesema Serikali Iko Katika Mchakato wa Kuhakikisha Wananchi Wanapata Huduma za Umeme, Maji, Mawasiliano, Afya Pamoja na Ujenzi wa Barabara za Lami Zinazounganisha Makao Makuu ya Mkoa wa Njombe na Wilaya Zake Kupitia mpango wa Matokeo Makubwa Sasa .
Rais Jakaya Kikwete Hii Leo Amehitimisha Ziara Yake ya Kikazi ya Siku Sita Kwa Kufanya Majumuisho ya Sehemu Zote Alizotembelea Katika Wilaya za Mkoa wa Njombe Huku Akiwapongeza Wananchi Kwa Kushirikiana na Serikali Katika Shughuli za Maendeleo
Hapo jana akielekea viwanja vya Liganga Rais Kikwete ,Wakazi wa vijiji vya Madope, Mlangali na Luana katika wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe, wamezuia msafara wa Rais Jakaya Kikwete na kumweleza kero zao mbalimbali ikiwemo ya kuidai serikali malipo yao ya mahindi iliyoyanunua kwa ajili ya kuhifadhi kwenye maghala ya taifa pamoja na kuwatafutia soko la mahindi kutokana na serikali kujaza maghala yake ya chakula cha ziada katika maghala yake, na kumtaka kuwajengea kwa kiwango cha lami barabara ya Itoni-Ludewa-Manda inayotoka Njombe kupita Ludewa Mjini hadi Manda.
Kero nyingine zilizotajwa na
wananchi hao ni kujengewa miundombinu ya mawasiliano, maji, umeme na maabara
katika maeneo yao
ili kuweza kupiga hatua kimaendeleo.
Matukio hayo yalitokea kwa nyakati
tofauti majira ya saa 5 asubuhi na saa 6 mchana wakati msafara wa Rais ukitoka Njombe kueleke wilayani Makete.
Kituko katika msafara huo ni pale
wakazi wa kijiji cha Mlangali walipousimamisha msafara huo huku wakiwa wamebeba
mabango yenye kuwasilisha ujumbe wa kero zao, likiwemo lililosomeka “Barabara kero tutakufa bila
kuona barabara ya lami, hatutaki mbolea ya minjingu tunataka DAP, miaka 50 ya
uhuru bado tunatumia vibatari na tuna kero ya kutolipwa hela za mahindi na
huduma ya maji kero” yaliyotosha kabisa kumfikishia ujumbe Rais Kikwete kwamba
wananchi hao wanahitaji nini.
Wananchi hao walisema pamoja na
kuiuzia serikali mahindi yao lakini mpaka sasa
wengi wao hawajapata fedha zao, huku wengine mahindi yao yakibaki ndani ya nyumba zao kutokana na
kukosa soko na hivyo kuhoji wakauzie wapi.
Pamoja na kero hiyo wananchi hao
wa Mlangali waliwasilisha kero la gari la wagonjwa (Ambulance) ambapo walidai
pamoja na kuletewa gari hilo
likimekuwa likikaa Ludewa mjini hali ambayo inawapa taabu pindi wanapohitaji
kuwahisha wagonjwa, na kwamba limekuwa likionekana katika kituo chao cha afya
pale tu wanapokuja viongozi wa kitaifa.
Hata Rais Kikwete alisema
serikali iko kwenye mpango wa kutatua changamoto hizo, ambapo hadi Disemba
mwaka 2014 itakuwa imejenga miundo mbinu ya umeme katika vijiji 74 vya wilaya
hiyo, maji vijiji 10 na minara ya mawasiliano katika vijiji vitano kikiwemo kijiji
cha Madope pamoja na kujenga zahati katika kijiji Luana, ujenzi ambao kwa
kuanza amechangia sh. 2 milioni pamoja na mabati 100, na kuongeza vijiji
ambavyo havitapa huduma hizo katika mpango wa mwaka huu visubiri awamu ya pili
ya utekelezaji wa miradi.
Kuhusu ujenzi wa barabara ya lami
kutoka Njombe-Ludewa-Manda (Itoni-Ludewa-Manda) alisema serikali iko kwenye matayarisho
ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kuwa iko katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi
ya CCM.
“Barabara ya lami tutajenga
lakini siyo leo, kwa sasa iko kwenye matayarisho na mchakato wake
utakapokamilika tutaanza kuijenga alisema,” Rais Kikwete.
Kuhusu madai ya mahindi
aliwaahidi wananchi hao kuwa fedha zao watalipwa muda siyo mrefu kuanzia sasa,
na kuwataka kuuza mahindi yao
yaliyobaki kwa taasisi binafsi kwa kuwa maghala ya taifa ya hifadhi ya chakula
yamejaa kwani yana uwezo wa kubeba tani laki 2.5 tu.
“Maghala yetu ya hifadhi ya
chakula yanauwezo wa kubeba tani laki mbili na nusu tu, kwa hiyo kwa sasa
tunatoa fursa kwa kampuni binafsi watusaidie kununua mahindi yenu, lakini fedha
zenu za mahindi mliyoutuuzia zitakuja na mtalipwa muda si mrefu na mimi
nitafuatilia,” alisema.
Akizungumza na wananchi wa Ludewa
mara baada ya kuzindua maabara ya kisasa katika hospitali ya wilaya ya Ludewa pamoja
na kuwaahidi kuwaletea vifaa tenganishi dawa na vifaa tiba, pia aliwaahidi
kuwaletea meli ambayo itasaidia kurahisha safari za majini katika ziwa Nyasa
kati ya wakazi ya tarafa ya Mwambao wilayani humo na Makete, wilaya ya Nyasa
mkoani Ruvuma na Kyela katika mkoa wa Mbeya.
Hata hivyo Mbunge wa Ludewa Deo
Filikunjombe leo alikuwa kivutio katika umati wa wananchi mjini Ludewa baada ya
kujitokeza na kumuomba radhi Rais Kikwete kwa mambo aliyomkwaza, na kwamba
mambo yote aliyomkwaza ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Ludewa
waliomtuma kuwawakilisha.
“Mh. Rais, baba yangu Kikwete
najua kuna mambo mengi nimekukwaza nazungumza wazi lakini nakuomba unisamehe
sana pale nilipokukwaza, ila najua katika maeneo yote niliyokukwaza ni kwa
ajili ya maendeleo ya wananchi hawa walionituma kuwawakilisha,” alisema.
Alisema pamoja na mambo hayo yuko
bega kwa bega naye katika kusimamia shughuli za maendeleo ya wananchi.
No comments:
Post a Comment