Wednesday, October 23, 2013
WANANCHI LUDEWA WAHAKIKISHIWA KUNUFAIKA NA RASILIMALI ZILIZOPO WILAYANI HUMO
WAWEKEZAJI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA TOKA CHINA WAKISUBIRI KUMPOKEA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. SOMA ZAIDI HAPAA
HUU MLIMA NI MLIMA WA MADINI YA CHUMA YA LIGANGA
PICHA YA PAMOJA RAIS AKIWA NA WAWEKEZAJI WATAKAOHUSIKA KUJENGA KIWANDA CHA KUFUA CHUMA HICHO PAMOJA NA MAWAZIRI MBALIMBALI AKIWEMO NAIBU WAZIRI WA MADINI.
RAIS KIKWETE AKIWA KATIKA KIJIJI CHA MUNDINDI NA HAPA ANAHUTUBIA MARA BAADA YA KUTEMBELEA MADINI YA CHUMA YA LIGANGA HAPO JANA
WANANCHI WA KIJIJI CHA AMANI KATA YA MUNDINDI WAKISIKILIZA HOTUBA YA RAIS
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete jana amehitimisha ziara yake ya siku tano mkoani Njombe ambapo pamoja na mambo mengine amesema serikali inatarajia kujenga chuo cha VETA katika kijiji cha Shaulimoyo ambacho kitasaidia kutoa elimu juu ya fursa zitakazokuwepo katika maeneo ya wawekezaji wa madini ambayo kiwanda chake kinatarajiwa kuanzi ujenzi wake mwaka 2014.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mundindi Rais Kikwete amesema kuwa serikali ilitangaza tenda ya kuanza uchimbaji wa madini hayo kwa kushindanisha na makampuni mengine ambapo kampuni ya china ya Hongdown group ndiyo iliyoshinda na itaanza kujenga kiwanda cha kwaajili ya kuchimba na kutengeneza chuma ujenzi unaotarajia kuanza february mwakani 2014.
Aidha Dkt Kikwete amesema kuwa rasilimali zilizopo katika machimbo ya migodi ya madini ya chuma itatumika kwa zaidi ya miaka sabini huku makaa ya mawe mchuchuma uchimbaji wake utatumika kwa zaidi ya miaka mia moja na ishirini ambapo upende wa liganga dola bilioni tatu zitawekezwa huku upande wa makaa ya mawe mchuchuma ikiwekezwa dola bilioni moja nukta saba na kwamba mapinduzi ya viwanda Uingereza yalisababishwa na chuma na hivyo Tanzania nayo itafanya mapinduzi hayo.
Aidha dkt Kikwete amesema kuwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa itakwenda kunufaika kwa kiasi kikubwa kwa kuingiza shilingi bilioni nane kwa mwaka ambapo fursa za ajira zaidi ya elfu 33 zitatolewa kwa vijana wa Ludewa na maeneo mengine wakitarajiwa kuajiriwa .
Mbunge wa Wilaya ya Ludewa Deo Filkunjombe ameishukuru serikali kwa kutenga pesa zaidi ya shilingi bilioni nne kwaajili ya ujenzi wa chuo cha VETA huku akiomba kuwekwa kwa utaratibu mzuri wa kuwahamisha wananchi waliko jirani na maeneo ya machimbo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment