Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, October 24, 2013

MKAZI MMOJA WA MTAA WA MATALAWE AMEUWAWA KWA KUPIGWA NA CHEPE KICHWANI NA MWENZAKE WAKATI WAKIFANYA KAZI ZA USAFI MJINI NJOMBE,CHANZO KUNYANG'ANYIANA CHEPE HIYO.


 RPC Mkoa wa Njombe ACP Fulgence Ngonyani akiwa ofisini kwake akizungumza na waandishi wa habari
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linamshikilia Maulid Mwalugoya  Mwenye Umri wa

Miaka 22 Mkazi wa Mtaa wa Matalawe Mjini Njombe Kwa Tuhuma za Kusababisha

Kifo cha William Mtokoma .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amesema Tukio Hilo

Limetokea Oktoba 23 Majira ya Saa Nne Kasorobo Asubuhi Eneo la Mtaa wa CCM

Mjini Njombe.

ACP Ngonyani Amesema   Tukio Hilo Limetokana na Ugomvi wa Kugombea Chepe

Kati ya Marehemu na Mtuhumiwa Wakati Wakifanya Kazi Ambapo Mtuhumiwa

Maulid Mwalugoya Alimkata Marehemu William Mtokoma Sehemu za Kichwani .
Katika Tukio Lingine Kamanda Ngonyani Amesema Mtu Mmoja Ambaye

Hakufamika Jina Lake Anaekadiliwa Kuwa na Umri wa Miaka 28 wajinsia ya kiume

Amekutwa Amefariki Huku  Mikono Yake Ikiwa Imefungwa Kamba na Mwili Wake

Kutupwa Ndani ya Mto Ruhuji.

ACP Ngonyani Amesema Mtu huyo Inasadikika Kuwa Ameuwawa na Watu

Wasiofahamika na Kuongeza Kuwa Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe Linaendelea na

Uchunguzi Dhidi ya Matukio Hayo.

No comments:

Post a Comment