Tuesday, October 1, 2013
WAZEE MKOANI NJOMBE WALALAMIKIA KUKOSA HUDUMA ZA MATIBABU BULE LICHA YA SERIKALI KUSEMA MATIBABU BULE KWA WAZEE
WANANCHI MBALIMBALI WA KATA YA UWEMBA WAKITOKA KANISANI KATIKA KANISA KATHOLIKI PAROKIA YA UWEMBA
NI MIONGONI MWA WAZEE NA WAZEE WATARAJIWA WAKIBURUDISHA UMATI WA WATAZAMAJI KWA MUZIKI WA NGOMA YA ASILI KATIKA KIKUNDI TOKA NJOMULOLE CHA MBETA GROUP
EDWARD MWALONGO AMBAE PIA NI DIWANI WA KATA YA UWEMBA AKIWA MGENI RASMI KATIKA SIKU YA WAZEE DUNIANI
WAZEE MBALIMBALI WAKIWA PAMOJA NA WAZEE WATARAJIWA WAKIMSIKILIZA MGENI RASMI
Kwa Mara Nyingine Tena Baadhi ya Wazee Katika Mji wa Njombe na Vitongoji Vyake Wameitaka Serikali Kutimiza Ahadi Yake na Kuisimamia Sera ya Wazee Ikiwemo Kupatiwa Matibabu Bure Pamoja na Pensheni.
Aidha Wazee Hao Pia Wametaka Kuthaminiwa na Kutambua Michango Yao Pamoja na Kushirikishwa Katika Shughuli Mbalimbali za Kijamii Huku Wakilalamikia Hali Ilivyo Kwasasa Kwani Wamedai Kutothaminiwa Licha ya Mchango Walioutoa Wakati wa Ujana Wao.
Wakiongea Kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani Yaliyoadhimishwa Katika Kata ya Uwemba Kwa Halmashauri Mji Wazee Hao Wamelalamiki Kitendo cha Kutopata Matibabu Bure Kama Ilivyoagizwa na Serikali na Kuongeza Kuwa Wamekuwa Wakipuuzwa Pindi Wanapofika Kwenye Vituo Vya Kutolea Huduma za Afya.
Hata Hivyo Wazee wa Hao Wamelishukuru Shirika Lisilo la Kiserikali la PAD Kwa Misaada Inayoitoa Kwa Wazee Hao Ikiwemo ya Kijasiriamali Pamoja na Kuanda Utaratibu wa Kutoa Vitambulisho Vya Matibabu.
Akijibu Hoja za Wazee Hao Mgeni Rasmi Katika Maadhimisho Hayo Edward Mwalongo Ambaye Pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Amewataka Wazee Hao Kufika Katika Vituo Vya Kutolea Huduma za Afya na Kuona Jinsi Vituo Hivyo Vinavyotoa Huduma Hizo Kwa Wazee.
Siku ya Wazee Dunia Huadhimishwa Oktoba Mosi Kila Mwaka Ambapo Mwaka Huu Maadhimisho Hayo Yamefanyika Kitaifa Wilayani Korogwe Mkoani Tanga Chini ya Kauli Mbiu Isemayo HATIMA YA WAZEE ITATEGEMEA UPATIKANAJI WA WASHERIA YA WAZEE NA PENSHEBNI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment