Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, October 2, 2013

COCODA YA KABIDHI BAISKELI 46 KWA WAHUDUMU WA KUJITOLEA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU NJOMBE VIJIJINI



 WAHUDUMU WA KUJITOLEA KUSAIDIA WATOTO YATIMA TOKA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE NA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE WAKIKABIDHIWA USAFIRI AINA YA BAISKELI
 MAAFISA MAENDELEO YA JAMII  WA WILAYA NA MJI WA NJOMBE WAKIKABIDHI BAISKELI KWA WAHUDUMU HAO


 AFISA MAENDELEO YA JAMII HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE BI.YOHANA KALINGA ALIYESIMAMA UPANDE WA KUSHOTO AKIZUNGUMZA NA MAPARO SOCIAL WA VIJIJINI

AFISA MAENDELEO YA JAMII WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH CHAMBACHAMBA AKIKABIDHI BAISKELI  KWA MAPARA SOCIAL

Shirika lisilo la kiserikali la COCODA mkoa wa Njombe jana limekabidhi baiskeli 46 kwa wahudumu wa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwa maeneo ya vijiji  wa kutoka halmashauri ya mji na wilaya ya Njombe zitakazowasaidia kuwafikia watoto mbalimbali katika maeneo wanakoishi na kuwatambua.

Wakizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli hizo  kwa  wahudumu wa kujitolea kutoka halmashauri ya mji na wilaya ya Njombe  maafisa maendeleo ya jamii wa mji bi Yohana Kalinga na Sarah Chambachamba wamesema kuwa kufuatia kutolewa kwa baiskeli hizo wahudumu hao wanatakiwa kuzitumia kwa umakini na kwa mahitaji yaliolengwa ambapo amesema anatengemea tatizo lililokuwa likiwakabili na kusafiri kwa miguu kwa umbali mrefu litakuwa limepungua na hivyo kuwafikia na kuwatambua watoto hao kwa urahisi.

Wamewataka wahudumu hao kuanzisha vikundi na  miradi itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi pamoja na kupatiwa fursa za mikopo huku wakitakiwa kuwa na mshikamano na kutotengana jambo litakalosaidia kupata kipato na kuwasaidia watoto hao huku wakisema kuwa kumbukumbu ni muhimu kuhifadhi na kuzifikisha katika halmashauri husika ili serikali nayo ione namna gani itawasaidia.

Kwa upande wao wahudumu kutoka halmashauri ya mji na wilaya ya Njombe wamepongeza shirika hilo kwa hatua waliofikia ya kuwakabidhi baiskeli hizo na kwamba zitawasaidia kuwafikia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kuahidi kwenda kuunda vikundi na miradi mbalimbali itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi ambapo wamesema hapo awali walikuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya kukosa usafiri kutokana na maeneo mengi kuwa mbali .

Awali akiwakaribisha maafisa maendeleo ya Jamii wa halmashauri ya mji na wilaya ya Njombe meneja wa shirika la COCODA mkoa wa Njombe bi.Mery Kahemele amesema kuwa shirika hilo limekabidhi vifaa hivyo kupitia mradi wa pamoja Tuwalee ambao unasimamiwa na Afri Care na kufadhiliwa na USA ambapo baiskeli 20 zimekabidhiwa kwa wahudumu wa halmashauri ya wilaya huku baiskeli 26 zikikabidhiwa kwa wahudumu wa halmashauri ya mji wa Njombe.


No comments:

Post a Comment