Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya APEC
Imehitimisha mafunzo kwa madereva wa Bodaboda Wilaya ya CHUNYA yaliyojumuisha
wahitimu wapatao 170 ambapo wamekabidhiwa vyeti na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya DIWANI ATHUMANI.
Mafunzo hayo ya siku saba ambayo yalifunguliwa na Katibu Tawala wilaya ya CHUNYA
SOSTEN MAYOKA ambaye amesema Mkuu wa wilaya DEODATUS KINAWIRO anaunga mkono
juhudi za waendessha pikipiki kwa kuunda umoja ili kujikwamua kiuchumi.
KINAWIRO ameahidi kutoa shilingi laki
tano kwa ajili ya kuimarisha kikundi hicho ili kuunda SACCOS ya waendesha
BODABODA na Halmashauri tjenga
vituo viwili vya maegesho ya pikipiki eneo la MAKONGOLOSI na CHUNYA mjini ili
kuondoa adha ya ukosefu wa vituo vya maegesho.
Kwa upande wake mkufunzi wa asasi ya
APEC RESPIRIUS TIMINYWA amesema kuwa changamoto inayoikabili asasi yake ni
kutojitokeza kwa madereva wa Bodaboda ili kupatiwa mafunzo licha ya kutumia
nguvu kubwa kuhamasisha.
TIMINYWA ameiomba serikali kuipa
asasi yake ruzuku ya mafuta ili iweze kuwafikia watu wengi na kutoa mafunzo ili
madereva wapate uelewa na kupunguza ajali za barabarani ambazo nyingi
husababishwa na uzembe.
Kwa upande wake Kamanda wa Poilisi
Mkoa wa Mbeya DIWANI ATHUMANI ameipongeza asasi ya APEC kwa kusaidia kutoa
mafunzo kwa madereva wa Bodaboda kwani kwa kiasi kikubwa imesadia kupunguza
ajali na pia Jeshi limepata mafanikio kupitia dhana Polisi Jamii na Ulinzi
shirikishi.
Aidha DIWANI amewaasa wahitimu kuwa
makini katika kazi zao ili
kuepukana na wizi wa pikipiki na mauaji kwa kutobeba abiria zaidi ya mmoja
kwani kufanya hivyo wanajihatarishia maisha yao lakini pia wayatumie mafunzo
hayo ili kuleta ueledi wawapo barabarani.
Mafunzo hayo pia yanafanyika pia
MKWAJUNI ambapo yamefunguliwa na Diwani wa Kata ya MKWAJUNI Mheshimiwa CHESCO
NGAIRO Ambaye aliwataka madereva wa bodaboda kujitokeza kwa wingi ili kupata
mafunzo hayo ambapo yatahitimishwa SEPTEMBA 3 mwaka huu.
KWA HISANI YA MBEYA YETU
|
No comments:
Post a Comment