Tuesday, October 1, 2013
SERIKALI WILAYANI MAKETE MKOANI NJOMBE INAENDELEA KUPAMBANA NA KILIMO NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA TAARAFA YA MATAMBA
HAPA MWENGE UKIWA KIJIJI CHA MANG'OTO TAYARI KWA KUKABIDHIWA WILAYANI MAKETE
MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE BI ESTERINA KILASI AKIJIANDAA KUKABIDHI MWENGE WA UHURU KWA MKUU WA WILAYA YA MAKETE
BAADA YA MWENGE KUKIMBIZWA WILAYA YA MAKETE NA HAPA UKIWA UMEKWISHA KUWASILI MAHALA PA KULALA MWENGE ENEO LA KATA YA MATAMBA TAARAFA YA MATAMBA
STIVIN SANGA MSIMAMIZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KWA MKOA WA NJOMBE AKIWA NA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA JUMA ALLY SMAI
KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAFA JUMA ALLY SMAI AKITOA HOTUBA AKIWA KATIKA KATA YA MATAMBA WILAYANI MAKETE JUZI 29
KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU SMAI AKIWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA CHUO CHA UFUNDI CHA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA ODEN VALLY FOSTER CARE WILAYANI MAKETE
Halmashauri ya wilaya ya Makete kupitia kitengo cha jeshi la polisi mkoani Njombe
imesema itaendelea kuteketeza na kuwakamata wanaohusika na kilimo cha uzalishaji wa
madawa ya kulevya jumla ya gunia sitini za bangi zinazokadiliwa kuwa na kilo elfu tatu na
mashamba la nusu ekeli la bangi ziliteketezwa.
Akisoma taarifa ya Utii kwa Rais katibu tawala wa wilaya ya Makete bwana Joseph Chaula
amesema kuwa kwa kushirikiana na jeshi la polisi mwezi januari mwaka huu jeshi la polisi
kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kuteketeza ekali tatu nukta tano sawa na zaidi
ya kilo elfu moja mia saba kumi na tano za bangi na mwezi july mpaka september mwaka
huu likifanikiwa kukamata gunia sita za bangi.
Katika ziara ya mwenge wa Uhuru mwaka 2013 wilayani Makete Jumla ya miradi sita
yenye thamani ya zaidi ya shiringi mia tatu sitini na tisa wilayani humo
imekaguliwa,kuwekewa mawe ya msingi na kufunguliwa katika mbio hizo huku wananchi
wakipongezwa kwa hatua hiyo waliofikia.
Miradi iliyopitiwa na mwenge wa Uhuru hii leo wilayani Makete ni pamoja na kuwekewa
mawe ya msingi katika ofisi ya kata ya Tandala iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni
36,nyumba za watumishi wa hospitali ya wilaya ya Makete uliogharimu shilingi milioni mia
124,ufunguzi wa Chuo cha ufundi mbalimbali cha shirika lisilo la kiserikali la Eden Vally
Foster Care iliyogharimu milioni mia 7,ofisi ya afisa taarafa ya Mangoma iliyogharimu
milioni 6o na bweni la wasichana katika shule ya sekondari Ipelele iliyogharimu milioni
98.
Akisoma risala fupi kwa mgeni rasmi kaimu mkuu wa shule ya sekondary Ipelele bwana
Goodluck Muyenze na mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Makete Dr Elk Myonga
wamesema miradi hiyo imetekelezwa kupitia miradi ya LCGD na MMAM huku ofisi ya
afisa taarafa ikijengwa kupitia fedha zilizotoka serikali kuu.
Akizungumza na wananchi wa taarafa ya Matamba wilayani Makete mkoani Njombe
kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa bwana Jumba Ally Smai amesema kuwa wananchi
wanatakiwa kutambua madhara ya utumiaji wa bangi na kwamba husababisha vijana
wengi kupoteza fahamu na hatimae kuwa vichaa na kusema kuwa jamii inatakiwa
kuepukana na tabia hiyo pamoja na kuwashauri wale wanaohusika na utumiaji wa dawa
hizo.
Aidha bwan Smai amesema kuwa utumiaji wa dawa za kulevya umekuwa ukipelekea vijana
wengi kujihusisha na matendo ya wizi ambapo pamoja na mambo mengine hali hiyo
imekuwa ikipelekea kuwepo kwa wazurulaji na kusababisha vijana wengi kuendelea kuwa
tegemezi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment