Wakristo Njombe Watamkumbuka Kwa Mengi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka
shada la maua juu ya kaburi ya Askofu Mstaafu, Mhasham Raymond
Mwanyika, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika leo katika Kanisa
Katoliki Njombe. Picha na OMR.
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya Askofu Mstaafu, Mhasham Raymond Mwanyika, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika leo katika Kanisa Katholiki Njombe.
Makamu wa Rais, Dkt Bilal, akiwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wa dini mbalimbali wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu.
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal Amewaongoza Waumini wa Dini ya Kikristo , Viongozi Mbalimbali wa Serikali na Chama Pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Njombe na Maeneo ya Jirani Katika Mazishi ya Mhasham Askofu Mtaafu wa Jimbo la Njombe Raymond Mwanyika Yaliyofanyika Hii Leo Katika Jimbo la Njombe
Akitoa Salam za Serikali Dkt. Bilal Amesema Taifa Litamkumbuka Marehemu Raymond Mwanyika Kwa Mchango Wake Aliyoutoa Wakati wa Uhai Wake Kwa Jamii Hasa Katika Kuhubiri Amani ya Nchi Huku Akiwataka Viongozi wa Dini Kuendelea Kumuezi Kwa Kuhubiri Amani na Utulivu wa Nchini.
Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mhashamu Askofu Thalalecisius Ngalalekumtwa Ambaye ni Askofu wa Jimbo Katholiki la Iringa Amemuelezea Marehumu Mwanyika Kuwa ni Miongoni Mwa Maaskofu Walioweka Historia ya Kanisa Kwa Kufanikiwa Kuanzisha Jimbo la Njombe Pamoja na Kushiriki Kikamilifu Katika Kufanya Kazi Kwa Kushirikiana na Serikali.
Amesema Kuwa Marehemu Mwanyika Ameongoza Jimbo la Njombe Kwa Muda wa Miaka 30 Tangu Kuteuliwa Mwaka 1972 Ambapo Mwaka 2002 Alistaafu Uaskofu Kwa Kufanya Mambo Makubwa ya Kijamii na Kwa Wakristo Wote.
Aidha Mwanyika Alifanikiwa Kuanzisha Parokia Jimbo Njombe,Alifanikiwa Kuanzisha Shule za Seminari za Kilocha na Matola Pamoja na Vyuo Mbalimbali vya Ufundi Chini ya Usimamizi Wake Hivyo Katika Kumsindikiza Kwake hiyo Itakuwa ni Kumbukumbu Kwetu.
Kwa Upande Wake Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi.Anne Makinda Amesema Kuwa Marehemu Askofu Raymond Mwanyika Alitoa Ushirikiano Mkubwa Katika Kujenga Shule Mbalimba za Kata na Shule za Misheni na Kwamba Wabunge wa Mkoa wa Njombe Kutokana na Majukumu ya Kiserika Waliyonayo Wameshindwa Kufika Kushiriki Katika Msiba huo.
Mhashamu Askofu Mstaafu Raymond Mwanyika Amezikwa Ndani ya Kanisa la Jimbo Katholiki la Njombe Baada ya Kufariki Kwa Tatizo la Kuharibika Kwa Damu Kutokana na Kutumia Dawa za Malaria Kwa Muda Mrefu Pamoja na Kupanuka Kwa Moyo.
No comments:
Post a Comment