Wednesday, October 30, 2013
WANANCHI WILAYANI NJOMBE WAKOSA IMANI NA MBOLEA ZA MINJINGU
WATAALAMU WA HALMASHAURI WAKISIKILIZA NA KUJIBU MASWALI MBALIMBALI YANAYOWAKILISHWA NA MADIWANI HAYO KWA NIABA YA WANANCHI WAO KATIKA KATA WANAZOTOKEA
DIWANI WA KATA YA LUPEMBE BI.TWILUMBA WAPALILA AKIWA NA MADIWANI WENGINE KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE LEO
Serikali Mkoani Njombe Imesema Itaendelea Kuishauri Wizara ya Kilimo, Chakula
na Ushirika Kubadili Matumizi ya Mbolea za Minjingu Mazao Kutokana na Wananchi
Wengi Kudai Kuwa Haifai Kwa Kilimo na Kwamba Mbolea Hiyo Inafaa Kwa Baadhi
ya Maeneo ya Wilaya ya Wanging'ombe .
Kauli Hiyo Imetolewa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Ernest Mkongo
Katika Siku ya Pili ya Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya
Njombe Kufuatia Madiwani wa Baraza Hilo Kuilalamikia Mbolea Hiyo ya Minjingu
Mazao Kuwa Haifai Kwa Matumizi ya Kilimo .
Awali Wakitoa na Wakichangia Hoja Mbalimbali Kwenye Kikao Hicho cha Siku ya
Pili Madiwani Hao Wameiomba Serikali Kuwahisha Pembejeo za Ruzuku na
Kuwashirikisha Pindi Pembejeo Hizo Zinapofika na Kuanza Kugawiwa Kwa
Wananchi.
Aidha Madiwani Hao Wameiomba Serikali Kuwaandaa Maafisa Kilimo wa Kata na
Wilaya Kwa Ajili ya Mashamba Darasa ya Majaribio ya Pembejeo Kabla ya
Kupelekwa Kwa Wakulima Kama Walivyofanya Kwa Mbolea ya Yala Ili Kuondoa
Hofu Kwa Wananchi.
Kwa Upande Wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Njombe Mhandisi Mkalimoto Sengayavene Amekiri Kuwepo Kwa Malalamiko
Kuhusiana na Mbolea ya minjingu na Kueleza Kuwa Halmashauri Hiyo Itaendelea
Kuwahimiza Maafisa Kilimo Kuandaa Mashamba Darasa Kwaajili ya Kuonesha
Mfano Kwa Wakulima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment