Tuesday, October 29, 2013
HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE IMEFANIKIWA KUKUSANYA SHILINGI BILIONI MBILI KWA KIPINDI CHA MWEZI JULY-SEPT MWAKA WA FEDHA WA 2013/2014
KAIMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA NJOMBE SHAIBU MASASI AKIONGOZA BARAZA LA MADIWANI HII LEO KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE AKIWA NA KAIMU MKURUGENZI NA KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE ERNEST MKONGO.
WAJUMBE WA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Imefanikiwa Kukusanya Shilingi Bilioni Mbili
Kutoka Mapato ya Ndani na Ruzuku Kutoka Serikali Kuu Katika Kipindi cha Mwaka
wa Fedha 2013 / 2014 Huku Mapato ya Ndani Pekee Yake ni zaidi ya Shilingi
milioni mia moja hamsini na nne Sawa na Asilimia 24 ya Makisio ya Makusanyo
Aidha Katika Kipindi Hicho Halmashauri Hiyo Imetumia Shilingi Bilioni 1.422 Kwa
Ajili ya Matumizi Mabalimbali Ikiwemo Kulipa Mishahara ya Watumishi ,Matumizi
ya Ada Pamoja na Michango ya Sekondari .
Akizungumza Wakati wa Kufungua Kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya
Wilaya ya Njombe Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri Hiyo Shaibu Masasi
Amewataka Madiwani wa Baraza Hilo Kuongeza Kasi za Ukusanyaji Mapato na
Kuyasimamia Pamoja na Kudhibiti Matumizi Mabaya ya Fedha Hizo.
Akitoa Salamu za Serikali Kwenye Kikao Hicho Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Njombe Ernest Mkongo Amewataka Madiwani Hao Kushirikiana Katika Kusimamia
na Kuhamasisha Shughuli za Maendeleo Katika Majimbo Yao.
Wakisoma taarifa za mapato na matumizi watendaji wa kata mbalimbali zilizopo
katika halmashauri ya wilaya ya Njombe wamezungumzia mafanikio na changamoto
zinazowakabi katika kata zao
Kwa upande wao wajumbe wa baraza la madiwani halmashauri ya wilaya walichangia
mawazo mbalimbali huku baadhi yao wakitaka kufahamu taratibu zinazotumika
kuwaajiri watumishi hususani walimu na kwamba baadhi ya maeneo kuna walimu
wengi kuliko maeneo mengine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment