Mwili wa kikongwe na mkazi wa kijiji hicho Jampany Mhamali(78) ukiwa nje kusubiria polisi
WATU
watano wameuawa kikatili katika matukio mawili tofauti yaliyotokea wilayani
Chunya mkoani Mbeya likiwemo moja lililosababishwa na imani za kishirikina
pamoja na wivu wa mapenzi.
Tukio
la kwanza lilitokea Oktoba 25 mwaka huu majira ya saa 2:00 usiku katika kijiji
cha Mpona kata ya Totowe tarafa ya Songwe ambapo kikongwe na mkazi wa kijiji
hicho Jampany Mhamali(78) akiwa njiani kurudi nyumbani akitokea kwenye kilabu
cha pombe za kienyeji alivamiwa na watu wawili wasiofahamika na kukatwakatwa
mapanga kichwani na mkono wake wa kulia hadi kufa.
Baada
ya wakazi wa kijiji hicho kupata taarifa za mauaji hayo walijikusanya wakiwa na
silaha za jadi ikiwemo mawe na kuanzisha msako mkali kwa kufuata nyayo za viatu
vya watu waliotuhumiwa kuhusika na baadaye wakafanikiwa kuwakamata watu hao
ambao hawakufahamika majina na kuanza kuwashushia kipigo na kuwaua wote wawili.
Watuhumiwa
hao walikutwa kilomita kumi kutoka eneo la tukio wakiwa wamejifungia katika
chumba namba tatu katika nyumba ya kulala wageni ya Hazole ilioko Malangali
kata ya Totowe wakiwa wameficha mapanga chini ya godoro yanayohisiwa kutumika
kwenye mauaji hayo.
Akizungumzia
tukio hilo, Mtoto wa Marehemu January Mhamali alisema wauaji hao walifika nyumbani
hapo siku tatu kabla ya tukio wakiwa na nia ya kuomba kazi ya kibarua cha
kulima mashamba lakini marehemu alisema hana lakini wao waliendelea kufika kila
siku huku wakipewa chakula.
Hata
hivyo wakati wakiendelea kupigwa watuhumiwa hao walikiri kuhusika na mauaji ya
kikongwe Mhamali na kueleza kuwa wao walitumwa na Maneno Adamson maarufu kwa
jina la Lyambo ambaye alikuwa akimtuhumu kikongwe huyo kuwa ni mchawi.
Wanachi
hao baada ya kuwaua watuhumiwa wawili walikwenda moja kwa moja nyumbani kwa
mtuhumiwa wa tatu aliyetajwa kuwaagiza watu hao lakini kwa bahati mbaya
hawakufanikiwa kumkuta kwani alikuwa amekwisha toroka.
Mujibu
wa mhudumu wa nyumba ya kulala wageni Salome Emmanuel (26) alikiri kuwapokea
wauaji hao na kwamba haikuwa mara ya kwanza kufika katika nyumba hiyo bali
waliwahi kulala siku za nyuma na kusahau panga ambalo mhudumu aliwatunzia na
kuwarudishia walipolihitaji.
Alisema
Siku ya tukio walitoka mapema katika chumba chao na kurejea majira ya saa nne
usiku na kuongeza kuwa baada ya kufika walipata huduma ya vinywaji kabla ya
kulala na ndipo wananchi wakiongozwa na mtendaji wa Kijiji cha Malangali
Yaredi Mwanguku walipofika na kuwasihi wafungue mlango.
Hata
hivyo Mtendaji huyo alipiga simu Polisi ambao walifika eneo la tukio wakiwa na
silaha na kuwasihi wauaji hao kutoka nje lakini walikaidi amri ya Polisi ndipo
wananchi zaidi ya 200 walipoamua kuvunja dirisha na kuanza kuwashambulia ambapo
mmoja alifia papo hapo na mwingine kukimbia umbali wa kilomita moja kisha
kukamatwa na kuuawa.
Wakati
wananchi wakiwashambulia watu hao Askari Polisi aliyejulikana kwa jina la Zefa
ambaye alikuwa akiwatuliza wananchi hao alijikuta katika wakati mgumu baada ya
kupigwa jiwe kichwani ikiwa ni ishara ya kumwondoa katika eneo la tukio.
Aidha
katika tukio la pili Adelina Philimon(45) mkazi wa kijiji cha Magamba
wilayani hapa na Wasiwasi Mwashiombo(28) mkazi wa kijiji cha Ipoloto Wilayani
Mbozi waliuawa baada ya kuteketea kwa moto.
Wapenzi
hao ambao kiumri ni sawa na mama na mtoto wake waliteketea kwa moto baada ya
nyumba waliyokuwa wamelala kuchomwa moto na mtu aliyetajwa kwa jina la Zacharia
Mwingila(39) mkazi wa Tunduma wilayani Momba.
Chanzo
cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi ambapo mtuhumiwa ambaye kwa sasa
anashikiliwa na polisi alifikia hatua ya kuchoma moto nyumba baada ya kumkuta
mpenzi wake akiwa amelala na mwanaume mwingine majira ya saa tano za usiku wa
oktoba 25 mwaka huu katika kijiji cha Magamba wilayani Chunya.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walisema mtuhumiwa huyo alianza kwa kuwachoma
na visu wagoni wake na ndipo alipoamua kuchoma moto nyumba nzima ambayo
iliwateketeza hadi kufa.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Mbeya,
Robert Mayala alithibitisha kutokea kwa matukio hayo yote mawili na kuisihi
jamii kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mikononi na pia kuishi kwa
kuwatuhumu wakazi wenzao wakiwahusisha na imani za kishirikina.
|
No comments:
Post a Comment