MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI BWANA EDWIN MWANZINGA AKITOA TAARIFA KWA WAJUMBE WA BARAZA LA MADIWANI
DIWANI KATA YA LUGENGE
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE AKIJIBIA BAADHI YA MASWALI YALIOHOJIWA NA WAJUMBE WA BARAZA LA MADIWANI KWENYE MKUTANO MKUU WA BARAZA HILO.
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE BWANA ISSAYA MOSES
WATAALAM MBALIMBALI WA HALMASHAURI YA MJI WAKIWA KWENYE MKUTANO HUO WA BARAZA LA MADIWANI
Madiwani wa halmashauri ya mji wa jombe wametakiwa kuwajibika katika kutekeleza majukumu yao ikiwemo kusimamia kazi ya ukusanyaji wa mapato ya halmashauri kwa kuhakikisha kuwa mianya ya ukwepaji wa kulipa mapato ya halmashauri inazibwa.
Akifungua mkutano wa baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa njombe hii leo, mwenyekiti wa halmashauri hiyo Edwin Mwanzinga amesema hadi kufikia robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2013/2014 asilimia ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ni asilimia 18.1 ambapo hadi kumalizika kwa robo hiyo halmashauri hiyo ilitakiwa kuvuka asilimia 25 ili kufikia asilimia 100 mwezi june mwaka 2014.
Amewataka madiwa kuona umuhimu wa pekee katika kutilia mkazo suala la ukusanyaji wa mapato na kwamba uzembe wowote utapelekea wataalam kushindwa kufuatilia na kusimamia miradi mbalimbali ya halmashauroi na kupelekea kuonekana kuwa halmashauri haitekelezi mpango mkubwa uliopangwa na wananchi ili kuwa na mafanikio makubwa.
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo wa halmashauri ya mji amesema kuwa halmashauri hiyo imetekeleza shughuli mbalimbali ikiwemo kuendesha mchakato wa kupitisha rasimu ya uanzishwaji wa mfuko wa afya ya jamii, kuendesha zoezi la upimwaji ili kukidhi viwango vya kupewa fedha za mradi wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha mabasi mjini njombe zoezi ambalo limeanza octoba 11 mwaka 2013.
Awali akitoa salamu za serikali kwenye kikao hicho mkuu wa wilaya ya njombe bi sarah dumba amewasisitiza madiwani kuongeza jitihada katika ukusanyaji wa mapato ya ndani pamoja na kusimamia matumizi yake ikiwa ni moja ya majukumu yao ili kuwezesha kutoa huduma bora kwa wananchi.
Aidha bi Dumba amesema wakati umefika kwa halmashauri ya mji njombe kuhakikisha inatekeleza sera na mipango ya halmashauri hiyo kwa kuhakikisha ujenzi wa kituo cha kukusanya na kuhifadhi matunda unatekelezwa.
Bi Dumba ameyasema hayo kufuatia msisitizo wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania katika ziara yake mkoani njombe hivi karibuni, kuutaka mkoa wa njombe kuwa kitovu kikubwa nchini katika kilimo cha matunda.
Hata hivyo bi Dumba ameitaka halmashauri hiyo kujipanga katika kufanikisha kilimo cha matunda, ili kutoa manufaa makubwa na ongezeko la kipato kwa wananchi na halmashauri.
Aidha ameitaka halmashauri hiyo kuangalia uwezekano wa kuwasomesha wataalam waliopo mahususi kwa ajili ya mambo ya matunda na mboga kwa lengo la kupata masoko ya ndani na nje ya nchi, kuwezesha kongamano la matunda na mboga kutekeleza malengo yake ya kubainisha na kuainisha ili kupata takwimu kamili za wakulima wa matunda.
Amebainisha kuwa hali hiyo pia itapelekea kupata idadi kamili ya miti ya matunda iliyopo, kuwawezesha wakulima,wafanyabiashara wa vitalu vya miche ya matunda kupata mbegu bora na aina za matunda akitolea mfano, parachichi na matunda mengine yanayozalishwa katika halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment