Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, October 18, 2013

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE LEO AZINDUA MKOA WA NJOMBE



 NGOMA YA MUGANDA TOKA LUDEWA WAKIBURUDISHA UMATI KATIKA UZINDUZI WA MKOA LEO


 MWENYEKITI WA CCM MKOA WA NJOMBE DEO SANGA AKISALIMIANA NA RAIS JAKAYA KIKWETE


RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIHUTUBIA WANANCHI WA NJOMBE KATIKA UZINDUZI WA MKOA WA NJOMBE HABARI TUNAKULETEA.........
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania dkt Jakaya Mrisho Kikwete jana amezindua mkoa wa Njombe ambapo pamoja na mambo mengine amesema kabla ya mwisho wa mwaka huu  serikali inatarajia kuanzisha bank ya wakulima itakayotoa mikopo kwa wakulima ili waweze kupata pembejeo zitakazowezesha  kupanua kilimo chao na kupata mikopo yenye masharti nafuu.

Akizungumza baada ya kufanya tendo la Uzinduzi wa Mkoa wa Njombe Dkt     Kikwete amesema  kuwa wananchi wanatakiwa kuongeza jitihada katika kilimo cha Matunda na kilimo cha mbogamboga na kwamba serikali itakipa mkazo maalum kilimo hicho ambacho kitasaidia kutatua tatizo la kiuchumi kwa mwananchi mmojammoja na kuongeza pato la taifa.

Aidha Dkt Kikwete amesema kuwa wananchi wa mikoa ya Iringa,Njombe na Mbeya wanayo fursa kubwa ya kujihusisha pia katika sekta ya ufugaji wa ng'ombe wa maziwa ambao  kwa mazingira ya joto hawastawi vizuri na kwamba inashangaza kuona wananchi hawatilii mkazo katika sekta hiyo na kuwahimiza kufuga ng'ombe hao kwa wingi huku akisema serikali pia italitilia mkazo hilo .

Akitolea ufafanuzi kuhusiana na tatizo la maji linaloukabili  mkoa wa Njombe Naibu waziri wa Maji Binilith Mahenge amesema kuwa  wizara ya maji imepanga kwamba ifikapo mwaka 2015 maji mjini Njombe watakuwa wamefikia asilimia tisini ya kuwafikishia huduma hiyo katika miji yote na kwamba kwa mkoa wa Njombe serikali imetenga kiasi cha shilingi  bilioni saba nukta sita na bilioni nne kwaajili ya kufikisha maji vijijini na bilion tatu nukta tano kwaajili ya kusogeza maji Njombe mjini  kutoka chanzo cha mto nyenga.

Hata hivyo amesema kuwa serikali ina mkakati wa muda mrefu ambao utatumia chanzo cha mto hagafilo ambao utagharimu bilioni arobaini na tisa  ambapo huduma za maji katika miji midogo serikali imetenga milioni mia moja ili kuongeza maji kupitia bwawa lililopo makambako pamoja na kuweka pampu kwaajili ya huduma hiyo huku ikiendelea kuombea kwa wahisani huku akisema Rais wa  Kikwete ameahidi kusaidia milioni mia sita kwaajili ya maji Makambako.

No comments:

Post a Comment