Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, October 16, 2013

JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE LINAWATAFUTA WATU WATATU KWA TUHUMA ZA KUMBAKA KWA ZAMU MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA KICHIWA WILAYANI NJOMBE



 RPC MKOA WA NJOMBE FULGENCE NGONYANI AKIWA OFISINI KWAKE AKITOA TAARIFA HIYO KWA VYOMBO VYA HABARI HAPO JANA.
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linawatafuta Richard Kaduma , Kaulete Lulambo na Fredy Makweta Kwa Tuhuma za Kumbaka Mwanamke wa Miaka 30 Mkazi wa Kijiji cha Kichiwi Wilayani Njombe.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Iliyotolewa Kwa Vyombo Vya Habari na Kusainiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgence Ngonyani Imesema Kuwa Tukio Hilo Limetokea Oktoba 13 Mwaka Huu Majira ya Usiku.

Taarifa Hiyo Imeeleza Kuwa Watuhumiwa Hao Walivamia Nyumbani Kwa Mwanamke Huyo na Kumbaka Kwa Zamu na Kwamba Mwanamke Huyo Anaendelea Vizuri.

Aidha Taarifa Hiyo ya Jeshi Imesema Kuwa Jeshi Hili Linaendelea na Uchunguzi wa Tukio Hilo Pamoja Kuwatafuwa Watu Waliohusika na Tukio Hilo Huki Likiwaomba Wananchi Kushirikiana na Jeshi la Polisi Kuwabaini Watu Hao.

Wakati Huo Huo Kamanda Ngonyani Amewataka Madereva wa  Magari na Pikipiki Kufuata Sheria za Usalama Barabarani na Kuwajali Watu Wengi Wanaotumia Barabara Ili Kuepusaha Ajali Zisizotarajiwa.

No comments:

Post a Comment