ENZI ZAKE MNAMO TAREHE 23 ALIPOFANYA MKUTANO NA WANANCHI WA MTAA WA KWIVAHA KATA YA NJOMBE MJINI MREHEMU LUPYANA FUTE.
Hayati Lupyana Fute Akizungumza Kwenye Moja ya Vikao vya Baraza la Madiwani Enzi za Uhai Wake.
Na Mwandishi Wetu.
Diwani wa Kata ya Njombe Mji Lupyana Fute Ambaye Pia Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Wilaya ya Njombe NEC Amefariki dunia Ghafla Jioni ya Leo Mjini Njombe .
Taarifa za Awali toka Kwa Mashuhuda wa Tukio Hilo Akiwemo Solanus Mhagama Amesema Kwa Mara ya Mwisho Marehemu Lupyana Fute Alimpigia Simu na Kumwambia Amtafutia Gari la Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji Baada ya Moto Kuzuka Kwenye Chumba cha Jengo la Ofisi yake Iliyopo Karibu na Tumaini Dispensari.
Bwana Mhagama Amesema Mara Baada ya Kufika Gari Hilo na Kufanikiwa Kuzima Moto Kwa Kushirikiana na Wananchi Uliokuwa Ukiwaka Kwenye Chumba Cha Kuhifadhia Vitu[STOO] ndipo Marehemu Alipoingia Ofisini Kwake Alikopotezea Fahamu.
Aidha Amesema Walipoingia Ofisini Kwake Walimkuta Marehemu Fute Akiwa Amepoteza Fahamu Huku Akiwa Amekaa Kwenye Kiti Ndipo walipomchukua na Kumupeleka Hospitali ya Kibena kwa matibabu zaidi ambapo baada ya kufika katika hospitali hiyo na kupatiwa vipimo vya kitabibu dr akasema amekwisha kufariki.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Edwin Mwanzinga Amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kwamba Taarifa Zaidi Zitaendelea Kutolewa.
No comments:
Post a Comment