Thursday, October 31, 2013
BAADA YA MAANDAMANO YA WAMILIKI NA MADEREVA WA MAGARI KUFIKA OFISI YA MKURUGENZI SAFARI ILIELEKEA MPAKA ENEO LA MAEGESHO BAADA YAKUAMULIWA NA KAIMU MKURUGENZI KWAMBA WAANDIKE MALALAMIKO NDIPO WAMPELEKEE AYAFANYIE KAZI.
HAPA SAFARI YAKUELEKEA KATIKA OFISI YA MKURUGENZI KUTOA MALALAMIKO YAO MADEREVA BAADA YA KUKUTANA NA WANAOKAMATA MAGARI YALIOEGESHWA KINYUME NA UTARATIBU.
HII NI OFISI YA MKURUGENZI HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE
KAIMU MKURUGENZI HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE AMBAE PIA NI AFISA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI HALMASHAURI YA MJI VENANCE MSUNGU.
KAIM MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE AKIZUNGUMZA NA MADEREVA HAO AKIWA OFISINI KWAKE KABLA HAWAJAENDA KWENYE ENEO LILILOPANGWA NA HALMASHAURI KWAAJILI YA MAEGESHO
HAPA WANAINGIA KWENYE ENEO LA MAEGESHO LA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE
HALI HALISI NDO HIYO UWANJA ULIOSHINDILIWA UNAFUKULIWA KWA MIKONO JAMBO AMBALO MADERAVA NA WAMILIKI HAO WAMESHINDWA KUAMINI NA KUENDELEA KUGOMA KUINGIZA MAGARI YAO KWA MADAI YANA TANI ZAIDI YA 30 HIVYO YAKIPELEKWA ENEO HILO HUENDA WAKAHARIBU MAGARI YAO JAMBO AMBALO WATAALAMU WA HALMASHAURI WAMELIPINGA KWAMBA HAIWEZEKANI KUHARIBIKA WAKIINGIZA MAGARI HAYO.
HAPA WAMILIKI NA MADEREVA WAKITHIBITISHA KAMA ENEO LINALODHANIWA LIMESHINDILIWA KAMA NI HABARI ZA KWELI NA HAPO WANAFUKUWA KWA MKONO NA MIGUU MAENEO MENGINE KUJUA KWELI WAMESHINDILIA.
MUHANDIS MKANGALA
HAPA WAMEMZUNGUKA MUHANDIS HUYO ILI ATOLEE UFAFANUZI KAMA ENEO HILO LIMESHINDILIWA AMA SIVYO
MHANDIS WA UJENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE BWANA IBRAHIM MKANGALA AKIHOJIWA NA MADEREVA HAO KATIKA ENEO LA MAEGESHO HILO
WAMILIKI WA MAGARI NA MADEREVA WAKIELEKEA KUKAGUA ENEO LA MAEGESHO WANALOTAKIWA KUEGESHA MAGARI YOTE YA MIZIGO
Wamiliki na Madereva wa Magari Makubwa ya Mizigo Hii Leo Wameandamana Hadi Ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Wakipinga Kitendo cha Kukamatwa na Kutozwa Faini Kwa Magari Yanayoshusha na Kupakia Mizigo Kwenye Maduka Mjini Njombe.
Wakizungumza Mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri Hiyo Wamiliki na Madereva Hao Wamesema Wanashangazwa na Kitendo cha Maafisa wa Usalama Barabani na Wataalam wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Kuanza Zoezi la Kuyakamata Magari Yanayoegeshwa Kinyume cha Sheria Hata Kwa Yale Yanayoshusha na Kupakia Mizigo Kwenye Maduka.
Wakielezea Sababu za Kutoegesha Magari Hayo Kwenye Eneo Lililotengwa Kwa Ajili ya Maegesho ya Magari Makubwa na ya Mizigo Wamiliki na Madereva Hao Wamesema Eneo Hilo Halina Miundombinu Inayokidhi Mahitaji ya Wamiliki na Madereva Hao.
Akizungumza na Wawakilishi wa Madereva na Wamiliki wa Magari Hayo Pamoja na Wataalam wa Halmashauri Hiyo Kabla ya Kwenda Maeneo ya Maegesho Hayo , Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Venance Msungu Amesema Sheria Inawataka Wamiliki na Madereva wa Magari Makubwa na ya Mizigo Kuegesha Eneo Lililotengwa Kisheria.
Bwana Msungu amesema kuwa eneo la maegesho limeshindiliwa na wahandis hivyo haoni sababu ya madereva na wamiliki wa magari kushindwa kwenda kuegesha magari yao eneo hilo ambapo baada ya kuona madereva hao hawajaridhishwa na majibu ya mkurugenzi na wanahitaji waongozane katika eneo husika la maegesho mkurugenzi huyo alimufuata Muhandis wa ujenzi akajibie madai ya madereva hao ambapo muhandis huyo aliruhusu kuendelea na zoezi la kupakia na kushusha mizigo katika maduka ya wafanyabiashara baada ya madereva kuonesha hali ya kutokubaliana na maelezo ya kiongozi huyo.
Akizungumza Kwenye Eneo la Maegesho Hayo Mhandisi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Ibrahimu Mkangala Amekiri Kuwepo Kwa Mapungufu Katika Eneo Hilo na Kuwaomba Wamiliki na Madereva Hao wa Magari Kuendelea Kushusha na Kupakia Mizigo Katika Maeneo ya Maduka Wakati Uongozi wa Halmashauri Hiyo Ikiendelea na Ukarabati wa Maegeshio Hayo.
Amesema kuwa swala la kuegesha katika eneo lililotengwa na halmashauri hiyo ni lazima litumiwe na madereva na wamiliki wa magari hayo ambapo kwa sasa wanaruhusiwa kwa kipindi hiki cha mpito kuendelea kushusha na kupakia mizigo katika maduka ya wafanyabiashara hao wakati halmashauri hiyo ikiendelea kuboresha miundombinu ya eneo la maegesho.
Kauli ya muhandis wa ujenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe bwana Ibrahim Mkangala ya kwamba wanaruhusiwa kuendelea na zoezi la kupakia na kushusha katika maeneo ya maduka ya wafanyabiashara imepelekea mgogoro kumalizika baada ya madereva hao kurizika na maelezo hayo na kwamba kusingesitishwa zoezi la kutoza faini na kuondoa magari yanayoshusha na kupakia mizigo kwenye maeneo ya maduka ya wafanyabiashara walipanga kuendelea kugoma kuingia kwenye yard ya maegesho hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment